Ndechumia
JF-Expert Member
- Jul 15, 2011
- 1,164
- 573
Mie ni mdau wa UTT liquid fund. Hii inafaa mtu ambae ana malengo Fulani so unakusanya pesa kidogokidogo. Wakati unasubiri upate kiasi unachokitaka ndo unaziweka huko utt. Ina faida ambayo siyo kubwa kivile, Kwa mwaka Si chini ya 12%, na Kwa mwezi ni kama 1%. Kwa mfano ukiwa na 10,000,000/- Kwa mwezi inazalisha Si chini ya 100,000.
Hii ilinisaidia wakati natafuta ka usafiri, nikawa Kila nikipata kiasi Fulani natupia humo, na hiyo faida inasaidia kuongezea mpaka nilivyotimiza lengo langu. Saving Acc bank Ina gharama so pesa haiongezeki. Fixed Acc inakupa mashart muda wa kuchukua fedha Yako labda miezi 6 au 12. Mimi sikuwa na chanzo Cha fedha kilichosawa, so sikuweza kujua ni lini nitafikia Malengo yangu.
Ukiwa na mfuko wa Liquid fund unaweza pata mpinga wako ndani ya siku 3 za kazi tangu umetumia maombi. Hakuna gharama za kuchukua pesa Yako, na sio lazima uchukue zote utachukua kiasi unachokihitaki. Pesa inawekwa kwenye Acc Yako ya Bank. Kama unachukua zaidi ya 2M utalazimika kujaza form maalum, chini ya hapo unafanya muhamala Kwa Simu tu chap.