Ila wee classmate ulichonifanyiaaaa...!!!!!!

Ila wee classmate ulichonifanyiaaaa...!!!!!!

Mahondaw

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
67,252
Reaction score
168,563
Aisee Wee classmate elfu mbili na........ Well known as Amri........d ni feki feki fekiiiiiii of all the fakes.
Umenitapeli hela yangu Japo ni kidogo mate kumbe bora nisingepingana na hisia zangu za kutaka kukupotezea tu Japo pesa nilikua nayo .
Kumbe ndokwanza wewe ni deiwaka mate na dereva magumashi tu huko Dar tena wa vi haisi sio wa long vehicles wala nini sio wa kwenda mombasa Uganda bukoba tanga nawala hata huko mwanza hujafika mate.
Kumbe ndokwanzaaa hio siku ulikua mbagala nasio kwamba ulikua njian porini kuelekea mwanza kupeleka wafungwa gereza gani sijui ambapo gari lilikuharibikia.
Kumbe utapeli ndo lifestyle lako mate hakuna cha long vehicles wala Rwanda. kumbe hata Shem wako Yulee dadake na rehema ushawahi kumtapeli mate.
Nilitaka kukunyima kwakua tulipotezana kitambooo tangu tumalize shule kwani sikuwa najua maisha yako
Lakini nafsi ikanisuta ikiniambia huyu mtu kaharibikiwa na gari porini sasa anataka amtumie mtu ampeletee kifaa akaniomba msaada kwani alikua anaelekea nilipo je nikimnyima wakaliwa na wanyama huko porini je?? Je wakivamiwa na majambazi nakuuliwa je? na wakidhuriwa kwa lolote je??? Si damu yake itakua imemwagikia mikononi mwangu??? Si nitabeba dhambi zake zote huyu??
Kwakua Linda alijitahidi kututafuta na kutuunganisha karibia ma classmates wote wahio elfu mbili na... Kina Monika zena rehema imelda Eva Adam mwanaenzi Allen Gody Frank Moze Vero rozi jack Angelina nawengine kidogo hio ikanifanya nikuamini kidogo kumbe u feki kabisa.
Ulihangaika sana na namba umepiga yako airtel salio likakata Voda likakata tigo likakata please recharge me ishirini kidogo si nikaamini eti shida imekukamata.
Kwakua sikuwa na salio kwenye mpesa yangu si Nikamwambia wakala mmoja jirani yangu atume ndani ya dakika 45 utatuma.. Mwee
Na ulipoipata ukanishukuru kabisa na kuniaminisha kuwa nisiwe na wasiwasi. Nilikutumia kabisa sms ya mpesa aliyonitumia wakala Revina ili uone kuwa nimefanya jitihada. Tangu hapo mpaka leo hata unapatikana hewani??? Voda tigo airtel kote hupatikani na kwa maana hiyo ndo ishakula kwangu mazima kulipa deni kunanihusu 100%.
Lazima nikutangaze kwenye group ili wote wajue kuwa wewe ni mtuhumiwa wewe una makosa ya madai kwa ashura na mimi ulipoona mwisho wa mwezi ukaona yes hapahapa.

Hivi kumbe hata mtu anayekufahamu fika anaeza kukutapeli?? Mi nikajua matapeli ni wale ambao hawakufahamu tu??? Aisee kuna dizaini ya watu wengine sio wa kuwasaidia kabisa hata alie machozi ya damu.
 
Kwa kua ushamjua alivyo mpotezee tu na msamehe...lipa deni achana nae...pole
 
Mimi kama ni msaada natoa tu, ila siyo kutegemea kulipwa deni.


Mimi mara zote narushwa tu
 
wazee wa asist. Pole dada kikulacho kinguoni mwako

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
classmate wangu bana wanamwingiza mjini wakati ndo kazaliwa huko huko mjini pole sana classmate mimi sina tabia kama izo bana. Nilipoona tu title nikajua ni mimi kumbe ni huyo mluga luga, sema tu classmate tuende kwa masharubu akamvimbishe zile gololi
 
Mmmhhh kwenye hiyo list umenitaja. Embu mlete kwenye grup tumchane huyo

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Back
Top Bottom