KERO Ilala Sokoni: Manispaa wanachukua Vizimba vya Wamachinga kisha wanawakodisha haohao Machinga

KERO Ilala Sokoni: Manispaa wanachukua Vizimba vya Wamachinga kisha wanawakodisha haohao Machinga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2026-07-23_23-58-04.jpg
Pale Ilala Sokoni kuna utaratibu umeanzishwa na viongozi wa soko na kutoka juu, wanataka Wamachinga au Wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wanamiliki vizimba au meza na baadhi ya maeneo, Eti wasiendelee kumiliki meza au vizimba badala yake manispaa ndo wamiliki meza za wamachinga.

Wakisha miliki vizimba na meza, Wataanza kuwakodisha hao hao wamachinga meza/vizimba kwa mkataba wa mwaka mmoja ukishindwa kulipia unanyang’any’wa meza anapewa mtu mwingine. Sasa wamachinga hawataki wanalalamika kwamba huo ni uonevu mkubwa na sio haki. Mtu ana kimeza chake alafu wachukue hao hao viongozi wakukodishe wakati kila wanatozwa ushuru
 
Back
Top Bottom