Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Pale Ilala Sokoni kuna utaratibu umeanzishwa na viongozi wa soko na kutoka juu, wanataka Wamachinga au Wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wanamiliki vizimba au meza na baadhi ya maeneo, Eti wasiendelee kumiliki meza au vizimba badala yake manispaa ndo wamiliki meza za wamachinga.
Wakisha miliki vizimba na meza, Wataanza kuwakodisha hao hao wamachinga meza/vizimba kwa mkataba wa mwaka mmoja ukishindwa kulipia unanyang’any’wa meza anapewa mtu mwingine. Sasa wamachinga hawataki wanalalamika kwamba huo ni uonevu mkubwa na sio haki. Mtu ana kimeza chake alafu wachukue hao hao viongozi wakukodishe wakati kila wanatozwa ushuru