Nimeweka hiyo Aya kwa maana sioni wapinzani wakiongea popote, kwa upande wa serikali najua zipo jitihada mfano kuna Kiwanda cha ngozi Moshi kinaendelea kujenga na kipo zaidi ya 90% kukamilika. Na ccm ipo na Sera ya viwanda, kuna viwanda vya usindikaji vinajengwa Muheza Tanga, kubangua korosho n. k. Hayo yote utayasikia mgombea akifika maeneo husika tega sikio.
Lakini la msingi ni kutungwa kwa sheria ya mifugo ya mwaka 2020 ambayo imerekebisha gharama za tozo ya chanjo ya mifugo, kutoa ruzuku ya dawa ya kuogesha mifugo na kuhimiza ufugaji wa kisasa Sera ambazo wapinzani hawana.
Mara fao la kujitoa wakulima na wafugaji wananitoa wapi? Au machinga na wafanyabiashara wadogo wananitoa nini?.
Sera ya kupunguza kodi ili iweje, ukope zaidi? Kufuta vitambulisho vya wajasiriamali halafu unafanyaje ukishafuta?.
Bado sana kuwa na wapinzani wa kupewa nchi, wa jipange.