Ila mkuu kishoka umekuwa ABSTRACT sana siku chache hizi, vipi umeshachukua uamuzi wa kujipima ubavu na mhishimiwa?
Msanii,
Siku moja nikiwa Dar, nilikuwa natoka msibani Kwembe narudi zangu Ubungo.
Tulipofika pale Mbezi Louis, tukaanza foleni ya kuja Dar tena kubwa na ilikuwa Jumamosi takriban Saa 12 na nusu Usiku.
Upande wa pili wa magari yanayotoka Dar kwenda mikoani, nako wakasimamishwa.
Sisi wa kwenda Dar tukaenda kinalenale taratibu, lakini utitiri wa msongamano unaongezeka pande zote mbili. Kufika pale Mbezi kwa Msuguri, hapakuwa na gari lolote kutoka Dar linalokwenda nje ya mji. Sisi nasi tukapigwa stop, hatuondoki.
Jamaa mmoja akadodosa, "Yawezekana mwenye nchi anarudi jijini"! Nikauliza anatokea wapi? wakasema anatokea kwenye mji wake Msoga ambao ni umbali fulani kutoka Chalinze.
Pindi si muda, msururu wa magari 22 ukapita fwap, mkukumkuku na vingora tele, roketi launcha na mbwembwe.
Mwinyi Fuadi akapita akitoka kwenye Kasri yake ya Msoga anaelekea Magogoni.
Sasa kumbe mwenzetu anapita ile zigizaga. Nilipokuwa nashangaa mbona hakuna magari kutoka Dar, kumbe wao walikuwa wanapisha njia, sawa na Yohana mbatizaji aliposema "yanyoosheni mapito"! na sisi kusimamisha ilikuwa ili huko mbele, msafara wake ucheze mayenu na kutamba ule upande wa kuingia Dar.
NIkauliza, kwa nini hatumii Helikopta kwenda Msoga?
Wakaniuliza wenzangu, "kwa nini atumie helikopta na ni gharama na rahisi kutunguliwa?"
Nikawauliza, je gharama ni ipi kati ya msafara wake kusimamisha mfumo wa Uchukuzi wa kuingia Dar kwa takriban masaa manne ambako hakuna kinachotoka wala kuingia Dar, magari yote yaliyosimama foleni na mafuta yanayoungua? Maana Msoga na Dar ni takriban masaa mawili!
Nikauliza tena la ziada la kuhusu usalama, nikasema "je usalama wake ukoje kama kwa mwendo huu wa mkukumkuku wa kilometa 100 kwa saa akatokea kiazi au duwanzi mmoja akachomoza akakatisha krosi kisha msafara wote upige breki za afanaleki, je si Taifa tutapigwa kofi la Kelb kama lile la Mzee Mwinyi?
Jamaa wakacheka, ksiha wakasema nilikuwa sahihi.
Sasa maana ya mimi kutoa hadithi hii ni hii, Raisi kila wikiendi huenda nyumbani Msoga, na zaidi barabara hufungwa na hakuna gari, basi au lori linapita. KUtoka Dar mpaka Msoga, kila kitu kinachotumia barabara kinatumia masaa ya ziada kumsubiri Mwinyi Fuadi apite.
Sasa kama yeye anaoina foleni kubwa hizo na jinsi msafara wake unavyoleta shida katika mfumo wa uchukuzi, je ni vipi tuseme kuwa Rais hajui kuwa barabara zetu ni ndogo, kuna foleni kubwa na zinachelewsha mambo mengi?
NIkajiuliza, ikiwa kuna msongamano mkubwa namna hiyo kisha labda kwa bahati mbaya kuna janga limetoea iwe ni Dar au Chalinze, je itatuchukua muda gani kufika kwenye janga au kama ni kupeleka Jeshi kulinda upande mmoja?
Hivyo bwana Msanii, katika ABSTRACT ya Mchungaji ni kuonyesha kuwa sisi kama Taifa tunakubali tuu mambo hata yale ya kipuuzi na yasiyo na msingi na kuyainua na kuyaweka kuwa ndio ya msingi!