MMJ,
Aksante sana kwa maelezo yako. Ni kweli Ilani ya Chadema haikutekelezwa kitaifa kwa vile hatukushika dola, na Ilani hutekelezwa kwa kodi ya Mwananchi na anayekusanya kodi na kupewa mandate ya kukusanya ni chama kilichoshinda ndiyo maana sifa au lawama zote huenda kwa chama Tawala at any given time. Hata hivyo, Ilani ya Chadema imekuwa Tested katika maeneo ambako Chadema ni "chama Tawala", kwa yale mambo ambayo ni local, na mengi ya hayo mambo yamekwisha kuchukuliwa na Taifa. Ukitaka kupima nenda Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambayo iko chini ya Chadema, Kwa sehemu, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ambaye inaongozwa kwa ushirikiano baina ya Chadema na CCM. Mathalan, Wilaya ya Karatu ndiyo iliyoanzisha ujenzi wa Sekondari katika kila kijiji na imeisha kukamilisha jambo hilo wakati Taifa liko bado ngazi ya Kata, ujenzi wa Zahanati katika ngazi ya Kijiji, na kutokea mwaka 2004 Halmashauri ya Karatu iliisha kukamilisha kazi hiyo na sasa tumevuka hata lengo kwani tuna zahanati hata kwenye ngazi ya vitongoji katika baadhi ya vijiji kutokana na jiografia ya eneo. Karatu ni mwalimu kwa Serikali ya CCM katika mengi, na mengi hayo bado hayafanyiki kitaifa, licha ya kuwa JK aliisha kuiga na kutangaza baadhi ya mambo hayo kuwa Sera yakitaifa. Hivyo, Chadema imekuwa Tested tayari kuliko chama kingine chochote cha upinzani na imefanya delivery ya tangible products ambazo zinaweza kuwa verified iwapo mtu ana nia njema.