Ile duniani ya ushindani wa wanasayansi imenda wapi mbona kimya?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Uvumbuzi siku hizi duniani umekwisha ? Au watu wenye akili nyingi wamepungua ?

Ile dunia wakati huo wanasayansi mbalimbali wakipigana vikumbo na mchaka mchaka wa kushindana kubuni formula, vitu na mambo mbalimbali ya kisayansi sasa kimya.

Ukisoma historia mchaka mchaka duniani enzi hizo wakina Isaac Newton, Albert Einstein, Nikola, Thomas Edison, Marie curie na wengine wengi

Dunia ilikuwa imejaa battle za wanasayansi wakipambana ile mbaya kugombea Nobel full fujo wengine mpaka fitina walikuwa wanafanyiana.

Dunia ya sasa hizo battle hazipo kimya, ni kwamba sisi sasa hatuna akili nyingi kama hao watu wa nyuma ?
 
Dunia ya wakati huo ilikuwa imejaa watabe wa Physics, Biology, Chemistry, Mathematics
 
Fika Silicon Valley hapo California ukajionee watu wanavyopambana na vumbuzi mbali mbali za ki teknolojia
 
Asaivi tuna historia ya sayansi..
Lakini pia uvumbuzi wa zamani ulikua unadili na Matatizo makubwa yaliyokua yakiisumbua dunia mfano,
Afya, Usafiri, Energy, mawasiliano..
Sasahivi ni modifications tuu ndani ya nyaja hizo.
 
Uvumbuzi siku hizi duniani umekwisha ? Au watu wenye akili nyingi wamepungua ?
Ile dunia wakati huo wanasayansi mbalimbali wakipigana vikumbo na mchaka mchaka wa kushindana kubuni formula, vitu na mambo mbalimbali ya kisayansi sasa kimya.

Ukisoma historia mchaka mchaka duniani enzi hizo wakina Isaac Newton, Albert Einstein, Nikola, Thomas Edison, Marie curie na wengine wengi

Dunia ilikuwa imejaa battle za wanasayansi wakipambana ile mbaya kugombea Nobel full fujo wengine mpaka fitina walikuwa wanafanyiana.

Dunia ya sasa hizo battle hazipo kimya, ni kwamba sisi sasa hatuna akili nyingi kama hao watu wa nyuma ?

Wanasayansi wapo...
 
Mkuu wewe umegundua nini mwenzetu, kama hujagundua kitu hebu tupe jibu, kwanini hugundui vitu kama wale wa mwanzoni
 
Fika Silicon Valley hapo California ukajionee watu wanavyopambana na vumbuzi mbali mbali za ki teknolojia
Kuna Great minds kama za wakati ule kama wakina Albert, Isaac, Nikola ?
 
Mkuu wewe umegundua nini mwenzetu, kama hujagundua kitu hebu tupe jibu, kwanini hugundui vitu kama wale wa mwanzoni
Mimi sio mwanasayansi sijabobea katika taaluma hiyo
 
Asaivi tuna historia ya sayansi..
Lakini pia uvumbuzi wa zamani ulikua unadili na Matatizo makubwa yaliyokua yakiisumbua dunia mfano,
Afya, Usafiri, Energy, mawasiliano..
Sasahivi ni modifications tuu ndani ya nyaja hizo.
Kweli mambo mengi huko nyuma wameisha fanywa na watabe wa sayansi sisi tunafanya modification tu
 
Wanasayansi wa kale walitufunza teknolojia ya kutengeneza makombora na kuya rusha ardhini, wanasayansi wa leo wana teknolojia ya kuzuia hayo makombora yasitue kwenye uso wa ardhi, hayo ni maendeleo ya sayansi na teknolojia
 
Wanasayansi hao hawakua wanavumbua vitu kwa sababu ya Nobel Prize. Hao unaowataja wamevimbua vitu kabla hata ya Nobel Prize kuanza.

Wanasayansi wa huko nyuma walishagundua na kuandika kanuni karibu zote za Dunia. Kilichopo sasa ni wanasayansi wa sasa wanaboresha tu hizo kanuni.
 
Hivi unajua kwamba mtoto wa high school sasaivi anaijua physics kuliko Isaack Newton na Albert Einstein?

Hata Newton akufufuka sasaivi atashangaa jinsi dunia ilivyokuwa. Na ukimuambia haya ni matokeo ya physics atapinga na kusema ni uchawi
 
Back
Top Bottom