Ile kauli ya Hayati Magufuli ya kwamba wapinzani wanachelewesha maendeleo ni ya kweli kabisa

dr namugari

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
10,466
Reaction score
18,206
Sijui Hayati Magufuli niseme ni nabii au aliona mbali hadi kutamka kauli ile, maanake mm binafsi nimekuja sasa kujua kuwa hawa jamaa ni watu wa ajabu sana kila kitu wanapinga na hata wamefika mbali kuzusha uongo ili mradi tu wazusshe taharuki katika jamii

Embu fikiria jana train yetu pendwa ya kisasa ya mwendokasi imekwama kutokana hitilafu ya grid ya taifa lkn wao wamekuja kwenye page zao na kuanza kuponda na kuzodoa ufanisi wa train hiyo na kudharau juhudi za mkurugenzi mkuu wa TRC bwana Kadogosa kwa kusema kuwa huyu ni mfungwa mtarajiwa, haya maneno ameyasema ex Mayor wa Ubungo Boniface Jacob

Mm binafsi Dr Namugari ni mdau mkubwa sana na ni mteja wa SGR kwa sasa hakika nimeona utofauti kati ya bus na train za mwendokasi, safari ya saa tano sasa ni saa mbili tu tena kwa bei nafuu zaidi, train iko kisasa sana haichoshi wala kuumiza mgogo na miguu na hakuna hatari yoyote ya kupata ajali wakati wote wa safari, hivi mnataka nini watanzania wenzangu?

Nashukuru sana Magufuli kwa kutuletea huduma muhimu hii ya kisasa kuwai kupatikana hapa nchini

CHADEMA wako tayari kuona train hii haifanyi kazi kuona bwawa la Nyerere linapasuka na kuleta madhara mkubwa wako radhi kuona hujuma ifanyike ili hizi miradi ya kimkatati ifeli na kufa tupate hasara

Jana nimewadharu sana Watu wa CHADEMA, mtu kama Hilda Newton, Boni yai wanakashifu mradi huu na kubeza juhudi za mwenda zake na Rais Samia Suluhu ktk kutekeleza miradi hii muhimu kwa uchumi wetu

Kama kweli CHADEMA ndio mko na siasa za namna hii hamtakaa kuungwa mkono na watanzania walio wengi kama ninyi ni kila kitu mnapinga na kubeza

Ni kweli mnaonewa na CCM kupitia Polisi ccm na pia mnanyanyaswa sana ila hili lisiende moja moja kuleta chuki kwa miradi yetu muhimu

Screenshot_20241205-104518.png
Screenshot_20241205-104230.png
Screenshot_20241205-104450.png
 
Ushawahi kuskia msemo wa adui Yako muombee Njaa. Siasa za TZ zimejaa uadui mwingi, ukifanya zuri litaonekana baya kwakua tu limefanywa na mtu asie wao.

Wao kwa wao wanapingana hadharani, wataweza kuwaacha wengine salama.
 
Wapinzani ni wa nchi zilizoendelea, wanakosoa kisomi kwa kutumia busara. Sio sisi akina kajamba nani.
 
Mimi nilifikiri Wapinzania ndiyo wamesababisha tatizo la Grid! Kumbe ni hayo?
Serikali ishughulikie changamoto za Umeme ili train zifanye kazi kwa ufanisi.
Tusitafute visingizio.
 
mweka mada hiyo avatar yako ni wewe huyo..?😅
 
Ushawahi kuskia msemo wa adui Yako muombee Njaa. Siasa za TZ zimejaa uadui mwingi, ukifanya zuri litaonekana baya kwakua tu limefanywa na mtu asie wao.

Wao kwa wao wanapingana hadharani, wataweza kuwaacha wengine salama.
Hawa jamaa nimewaona wajinga sna kwa kila kitu kwao iwe batili
 
Mimi nilifikiri Wapinzania ndiyo wamesababisha tatizo la Grid! Kumbe ni hayo?
Serikali ishughulikie changamoto za Umeme ili train zifanye kazi kwa ufanisi.
Tusitafute visingizio.
Ndio hvyo serekali inafanya kaz zake kwa weledi mkubwa changamoto hzo ni za kawaida
 
lakini walisema umeme hata ukikatika hautaathiri ufanisi wa train!nadhani ndo wanachohoji hao unaowaita wapinzani mkuu!!!embu jibuni hoja yao hyo then tuone wao watasemaje
 
Hpn siwezi kuwasemeha trc ila tuwe na subira mambo yatakaa tj Sawa hv vichangamoto siyo za kudumu
 
Watanzania wameshawaadhibu kwenye serikali za mitaa wanasubiri watoe tena adhabu kwenye uchaguzi mkuu 2025.
 
Wao kusema hivyo kunachelewesha vipi nchi mkuu? Na je toka wapinzani wapo pembeni kipi cha kutisha kilifanyika mkuu?
 
Sijui Hayati Magufuli niseme ni nabii au aliona mbali hadi kutamka kauli ile, maanake mm binafsi nimekuja sasa kujua kuwa hawa jamaa ni watu wa ajabu sana kila kitu wanapinga na hata wamefika mbali kuzusha uongo ili mradi tu wazusshe taharuki katika jamii

Embu fikiria jana train yetu pendwa ya kisasa ya mwendokasi imekwama kutokana hitilafu ya grid ya taifa lkn wao wamekuja kwenye page zao na kuanza kuponda na kuzodoa ufanisi wa train hiyo na kudharau juhudi za mkurugenzi mkuu wa TRC bwana Kadogosa kwa kusema kuwa huyu ni mfungwa mtarajiwa, haya maneno ameyasema ex Mayor wa Ubungo Boniface Jacob

Mm binafsi Dr Namugari ni mdau mkubwa sana na ni mteja wa SGR kwa sasa hakika nimeona utofauti kati ya bus na train za mwendokasi, safari ya saa tano sasa ni saa mbili tu tena kwa bei nafuu zaidi, train iko kisasa sana haichoshi wala kuumiza mgogo na miguu na hakuna hatari yoyote ya kupata ajali wakati wote wa safari, hivi mnataka nini watanzania wenzangu?

Nashukuru sana Magufuli kwa kutuletea huduma muhimu hii ya kisasa kuwai kupatikana hapa nchini

CHADEMA wako tayari kuona train hii haifanyi kazi kuona bwawa la Nyerere linapasuka na kuleta madhara mkubwa wako radhi kuona hujuma ifanyike ili hizi miradi ya kimkatati ifeli na kufa tupate hasara

Jana nimewadharu sana Watu wa CHADEMA, mtu kama Hilda Newton, Boni yai wanakashifu mradi huu na kubeza juhudi za mwenda zake na Rais Samia Suluhu ktk kutekeleza miradi hii muhimu kwa uchumi wetu

Kama kweli CHADEMA ndio mko na siasa za namna hii hamtakaa kuungwa mkono na watanzania walio wengi kama ninyi ni kila kitu mnapinga na kubeza

Ni kweli mnaonewa na CCM kupitia Polisi ccm na pia mnanyanyaswa sana ila hili lisiende moja moja kuleta chuki kwa miradi yetu muhimu

View attachment 3169405View attachment 3169406View attachment 3169407
Mtakuja taratiibu mkiimba pumbav zenu nyie
 
Kwani wapinzani ndo walikata umeme?

Majimbo yote Tanzania yanaongozwa na wabunge wa CCM mbona hatuoni hayo maendeleo? Jimbo la ukonga lipo hapa hapa Dar lakini bara bara hazipitiki au lina mbunge wa upinzani? 😅
 
Back
Top Bottom