Ile ndege ya ATCL iliyopeleka nyama ya mbuzi Oman haiwezi kupeleka minofu ya Sangara Ulaya?

Ile ndege ya ATCL iliyopeleka nyama ya mbuzi Oman haiwezi kupeleka minofu ya Sangara Ulaya?

Serikali haina shamba la maua Wala kiwanda Cha kusindika minofu. Waliokodi hizo ndege ni wawekezaji wenyewe.
Ni vigumu kufanya kazi na ATCL maana ghafla unaweza kukuta wameitelekeza bidhaa yako Kisha ndege imeenda Dodoma kubeba makada wa CCM
Yaani hili ndio jibu sahihi. Hivi wakati ule viwanda vya samaki vinasafirisha minofu na mandege yale ya Urusi serikali ilihusika na mikataba ya ndege zile? Waweke wazi sababu ya kusitishwa kwa safari zile!

Serikali hii inapenda sana kusema uongo bila aibu. Ndege hizo zinafanya kazi na viwanda sio serikali Ila wanatafuta tuu sifa mambo yakiharibika wanakimbia.

Awali ndege za Urusi zilizuiwa baada ya kujulikana kuwa zilikuwa zinapeleka silaha huko Congo na Angola kwa waasi na wakati wa kurudi zinapitia samaki. Kashfa hiyo iliharibu biashara hiyo. Sasa Covid19 imeyafanya mashirika hayo AirRwanda na Ethiopia kuona wanaweza kufanya biashara hiyo na kufanya makubaliano na viwanda. Lakini ATCL hawatakiwi maana sio reliable kibiashara.
 
Pia ndege za ATCL hazina uhakika wa kurudi nchini zikienda ughaibuni.
Tuna watu wengi huko nje wanatudai, ndege ikienda tu huko inadakwa
Duh, ndege inatuwa Athens kuongeza mafuta kisha inakamatwa ikiwa na mzigo wako wa samaki tani 40 za kwenda Copenhagen unafanyaje? yaani deni lisilokuhusu linakuharibia biashara? Nani anataka hayo?
 
Ayo Mashirika yana vibali kwenye izo njia kwa muda mrefu na hayachukui minofu ya samaki kutoka Tanzania pekeyake, kuna mizigo mingine mingi wanayo peleka pamoja na abilia. ATC bado hawajapewa iyo njia, ata wakipewa leo inabidi watangaze ili watu/kampuni zinazotaka kupeleka mizigo huko ziombe nafasi. Ndege sio babaji kwamba dereva ana amka na kwenda njia yoyote kutafuta abiria. Njia za ulaya zina ushindani mkubwa inabidi kujipanga sio kukurupuka.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kule tulikopeleka nyama ya mbuzi tuna kibali na tumepewa ile njia!

Nimekuelewa.
 
Nadhani vibali vya kuruka ATCL kwenda huko Ulaya ndio itakuwa shida kubwa………...Haiingii akilini waiache ATCL waingie huko Rwandair na Ethiopian Airline.
 
  1. Hizo ndege za abiria zinazo beba cargo, huwa zinakodiwa na cargo transporters
  2. Ndege ya ATCL pia iliwahi kukodiwa kupeleka mbuzi Dubai
  3. Ndege za wenzetu, wamevifugua viti ili kupata nafasi kubwa zaidi na kubeba mzigo mkubwa.
  4. Sisi tulibebesha mzigo kwa kuweka vi parcels kwenye viti.
  5. Gharama ya kurusha mdege mkubwa wenye mzigo mdogo ni kubwa kuliko gharama ya kurusha ndege ndogo yenye mzigo mkubwa.
  6. Hivyo hao transporters wana opt kukodisha Rwandan Air na Ethiopian Air kuja nchini kwetu kubeba mizigo yetu huku ile midege yetu imejidodea pale Airport huku sisi tukiangalia na kushangilia
  7. Sio kuwa Tanzania hatuna uwezo huo, bali hata bila ya janga la Corona, ATCL was operating on loss kwasababu bado hatuna watu wenye uwezo na akili ya ku run a successful airline business profitably
  8. Huu mtindo wa kukimbilia kununua midege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi bila kwanza kuwa na business plan, haya ndio matokeo.
  9. Hata hivyo, tusiilaumu sana ATCL, janga hili la Corona lime destabilize airline industry duniani kote mashirika kibao yamepunguza wafanyakazi kwa kushindwa kuwalipa while doing nothing, lakini sisi hatujapunguza mtu.
  10. Na kwenye usafirishaji wa mizigo, pia ATCL inajitahidi jitahidi tunapeleka cargo Comoro twice a week kwa bombardier.
P
Acha kudanganya watu , Ethiopian airlines wana ndege za mizigo hawafanyi biashara za kufungua Viti Kama Atcl.Pia shirika kubwa la ndege Kama Ethiopian airlines wana cargo division Kama una mzigo unawaona mwenyewe
 
Serikali haina shamba la maua Wala kiwanda Cha kusindika minofu. Waliokodi hizo ndege ni wawekezaji wenyewe.

Ni vigumu kufanya kazi na ATCL maana ghafla unaweza kukuta wameitelekeza bidhaa yako Kisha ndege imeenda Dodoma kubeba makada wa CCM
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom