BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Wavulana wanahitaji mifano ya kiume. Wanahitaji baba anayewaongoza kwa kielelezo na kwa upole lakini anayewatia moyo kwa uthabiti. Uadilifu ni muhimu kwa wavulana. Wanaitikia vyema nidhamu iliyo thabiti, ya uaminifu na ya haki.
Swahaba wa Mtume (s.a.w) aitwae `Umar alikuwa akitembea na mtoto wake Abdullah. Baba anatakiwa kuongozana na kijana wake wa kiume ikiwezekana hata kazini anaweza kwenda nae siku moja moja na kumpatia majukumu madogo madogo.
Baba anatakiwa kushiriki na kumfunza kijana hadithi nzuri kutoka kwenye Qur'an pamoja na visa vya wanaume wema waliotangulia. Baba lazima atenga muda kila siku kwa ajili ya kuwafundisha vijana wake maisha kwa matendo, Baba anatakiwa kuwapa majukumu watoto wake wakiume waliofikisha miaka 7.
Majukumu mbalimbali kama vile ununuzi wa LUKU na kuingiza Luku, kulipia bili za maji na kuzisoma hizo risiti kwa sauti mwanzo mwisho na umkabidhi azihifadhi. Usafi wa mazingira nje ya nyumba, kutunza bustani na mifugo ya nyumbani, mtoto wa kiume lazima afahamu hayo. Wape majukumu ya kuzunguka nyumba Kufuata maelekezo na kumaliza kazi ni ujuzi muhimu sanakatika kujifunza. Mpe mwanao kazi ya kawaida kila siku. Mtoto wa kiume ndio anatakiwa akupatie summary fupi ya taarifa ya habari iliyokupita.
Mbaya sana mtoto wa kiume chini ya miaka 7 kutazama tamthilia za mapenzi, Sawa na wasichana, wavulana wana hisia pia na hatupaswi kuwatia aibu katika hilo.
Kaka mdogo wa Anas bin Malik alikuwa akicheza na ndege mdogo. Mtume ﷺ alikuwa akimkaribia mtoto mdogo na kumuuliza: ❞❝“Ewe Abu Umair! Ndege wako mdogo amefanya nini leo?”❞ Siku moja ndege mdogo alikufa. Kijana huyo alihuzunika, hivyo Mtume wa Rehema akaenda kumtembelea, kumliwaza na kumtia moyo.
Wazazi wengi hawapendi fujo wala kelele zinazotokana na michezo ya watoto wakiume. Ni muhimu kukubali hilo na usiwe mzazi mwenye nidhamu kila wakati.
Japo wengine hupinga. Lakini haipendezi mtoto wakiume kuingia jikoni kupika ikiwa kuna mabinti wa kike ndani, haipendezi mwana wa kiume kuosha vyombo ikiwa kuna mabinti wakike. Katika nidhamu tunafundisha kwamba dada anatakiwa kufua nguo za kaka yake. Katika swala la uchumi tunafundishwa kwamba mara moja moja mpe mwanao wa kiume pesa ndogo ndogo (Change) zinazobakia akuhifadhie na uwe tayari kumuomba wakati wowote ule. Na katika hatua nyingine anapofanya kitu kizuri mpongeze.