Ili Kuboresha Elimu Tanzania, sheria hii ipitishwe haraka

Kagalala

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
2,403
Reaction score
1,133
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kushuka kwa kiwango cha elimu katika nchi yetu hasa katika matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha Nne na Sita. Ni kweli kuna matatizo mengine ambayo yanasababisha swala hili kutokea lakini jambo ambalo halipingiki ni Walimu kuwa na mgomo baridi na serikali kuendelea kutowajali walimu. Vile vile kumekuwa na uhuru wa kuanzisha shule binafsi ambazo sidhani kama zinasaidia katika kuwainua Watanzania wa kiwango cha chini ambao ndiyo asilimia kubwa ya idadi ya watu nchini.
Viongozi serikalini wamesahau umuhimu wa shule za Serikali na hili linatokana na watoto wao kutosoma katika shule hizo. Napendekeza itungwe sheria ambayo inazuhia watoto wa viongozi wa serikali kupeleka watoto wao katika shule binafsi. Hili litasaidia vingozi hao kuwajali walimu wanaowafundisha watoto wao katika shule za serikali na mkazo utawekwa kuziboresha na hatimaye kuboresha elimu nchi.

Sheria hii iwabane
Afisa Elimu wa Kata
Afisa Elimu wa Tarafa, Wilaya, Mkoa
Mkuu wa Wilaya, Mkoa
Wabunge wote
Mawaziri, Manaibu wao na Watendaji wakuu Wizarani
MKUU WA NCHI (Ni kashfa kwa mkuu wa nchi kusomesha mtoto wake shule binafsi)

Nawakilisha
 

Mimi nafikiri swala sio kuwabana viongozi, ila sera zenyewe zitajieleza. Kwanza, jiulize ni kwanini tuna standards mbili za Elimu ndani ya nchi moja?

I t is very obvious kwamba moja ni kwa ajili ya viongozi wakubwa serikalini na matajiri, na hii nyingine ni kwa ajili ya walalahoi.
N aukweli usiopingika unaonyesha wazi kwamba as long as zile za watoto wa wakubwa zinafanya vizuri (GROUP A), why bother on the government schools?

Worse still, viongozi wanamiliki shule. Mfano mzuri ni Naibu Waziri wa Elimu ambaye ana shule pale Mbeya..Je hapa hakuna mgongano wa kimaslahi kweli?

Hivi kunahaja yakuwa na serikali inayoendekeza double standards kwenye Elimu, na vingozi wake wakionyesha 100% propensity to one wing?
 

Ni kweli kabisa haya mambo ya Mawaziri kuwa na shule zao ndo yametufikisha hapa. Hii sheria inabidi itanuke mpaka kuwabana viongozi wa serikali kumiliki shule binafsi. Hili swala la elimu ni bomu ambalo litalipuka siku si nyingi. Gap la mwenye nacho na wasiokuwa nacho inaendelea kukua na hii ni hatari
 
aliyewahi kuwa waziri wa elimu Mungai anashule zake pale mafinga na zinaitwa hivyohivyo mungai hapo ndo ujue tuna aina gani ya viongozi wakiwa madarakani
 
Serikali imejenga shule kwa kila kata, kinachofuata ni kupeleka walimu na vifaa stahili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…