Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kushuka kwa kiwango cha elimu katika nchi yetu hasa katika matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha Nne na Sita. Ni kweli kuna matatizo mengine ambayo yanasababisha swala hili kutokea lakini jambo ambalo halipingiki ni Walimu kuwa na mgomo baridi na serikali kuendelea kutowajali walimu. Vile vile kumekuwa na uhuru wa kuanzisha shule binafsi ambazo sidhani kama zinasaidia katika kuwainua Watanzania wa kiwango cha chini ambao ndiyo asilimia kubwa ya idadi ya watu nchini.
Viongozi serikalini wamesahau umuhimu wa shule za Serikali na hili linatokana na watoto wao kutosoma katika shule hizo. Napendekeza itungwe sheria ambayo inazuhia watoto wa viongozi wa serikali kupeleka watoto wao katika shule binafsi. Hili litasaidia vingozi hao kuwajali walimu wanaowafundisha watoto wao katika shule za serikali na mkazo utawekwa kuziboresha na hatimaye kuboresha elimu nchi.
Sheria hii iwabane
Afisa Elimu wa Kata
Afisa Elimu wa Tarafa, Wilaya, Mkoa
Mkuu wa Wilaya, Mkoa
Wabunge wote
Mawaziri, Manaibu wao na Watendaji wakuu Wizarani
MKUU WA NCHI (Ni kashfa kwa mkuu wa nchi kusomesha mtoto wake shule binafsi)
Nawakilisha