chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Watanzania, au watu wengine huelewa kwa kuona kuliko kuambiwa. Mtu akiona kitu,kinalainisha moyo wake na anabadilika kimsimamo na kuelewa,kisha kutetea kwa nguvu alichokielewa.
Ili wananchi waelewe serikali ina maanisha kuhusu tozo za miamala,nashauri jambo moja.
Serikali iandae miradi ya mfano,miradi ya kisasa,bora kabisa kwa viwango, ya shule,vituo vya afya na maji,kwa kila mkoa au wilaya, nzuri kabisa ili ziwe tofauti na zilizopo kwa kila kitu iendane na upekee was tozo.
Miradi hii itakuwa inaisemea dhamira ya serikali,na itafanya serikali ipunguze kujieleza kuhusu dhamira yake, miradi hii ijisemee na iisemee serikali, hata mwananchi akipita mahali anasema loooh! Serikali imefanya jambo kubwa kijijini/wilayani/mkoani kwetu.
Miradi hii inapojengwa kuwe na ushirikishwaji was viongozi was eneo husika katika kila hatua, wakishirikishwa,hawa watakuwa mabalozi wazuri wa dhamira ya serikali, na wataisemea kwa kila hali,hapa namaanisha viongozi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji, NGO, vyama vya akina mama na vijana. Na waelezwe kinagaubaga kuwa fedha zinazojenga miradi hiyo ni mgao wa tozo ya miamala,hii itapeleka mrejesho kuwa alaaa, kumbe zile pesa walizokatwa zinerudi kwao kwa mfumo wa miradi ya maendeleo.
Sio mkandarasi aende tu saiti na kuanza kazi, kikao cha kijiji kiitishwe, au mtaa, waelezwe hayo.
Pia iwepo kamati ya kitaifa ya kudhibiti pesa hii, kamati ya watu wachache powerful, na pia kamati ya mkoa, ambayo itafatilia kila senti inayopelekwa.
Pia iandaliwe namna ya kutambua mradi wa kuanza nao na kumaliza nao kiuwiano kimkoa,kiwilaya na kitaifa, kikata na kijiji, iwepo schedule kabisa/jedwali linaloonyesha kimkoa, tunaanza na kijiji kipi, mtaa upi, baada ya muda gani tunaenda wapi, kila kijiji/mtaa ujue zamu yake, sababu za mtaa mmoja kuanza na mwingine kusubiri. Hii itapunguza tozo hizi kutumika tu kwenye maeneo ya wanasiasa wakubwa.
Miradi ya mfano ianze haraka kwa angalau wilaya mbili kila mkoa, kadri fedha itakavyoruhusu, na ikamilike ikibidi ndani ya miezi mitatu, idara ya habari maelezo na maafisa habari, kila wiki/wiki mbili wanaenda saiti, wanaandaa documentaries zirushwe katika TV, redio kuonyesha jamii kwamba miradi ina faida, hata wanaoipinga wataanza kunywea, na itapata support ya jamii.
Yachaguliwe maeneo yenye kugusa kwa haraka maisha ya wananchi, senta zao kubwakubwa ambako wakikutana, wanakuwa wanaiona miradi hiyo ya afya, elimu, barabara, maji.
Wakati tozo za mafuta kwa ajili ya TANROAD zinaanza, wananchi walilalamika sana, lakini walipoona barabara, nafsi zao zikatulia, na ilitangazwa kwelikweli katika TV na ilionekana hata kwa macho.
#kaziiendelee
#Code SSH2025