Ili kuepuka kipigo cha mbwa koko tarehe 20/4, naomba Simba ianze na kikosi hiki

Ili kuepuka kipigo cha mbwa koko tarehe 20/4, naomba Simba ianze na kikosi hiki

Bando la wiki

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2023
Posts
911
Reaction score
3,017
Mwenendo mbovu wa timu ya Simba, sisi mashabiki ndio tunapata shida huku uraiani.
Wachezaji wa simba zaidi ya 50%, wamechoka wako nje ya form; kwa kifupi wanajivuta kama konokono wawapo uwanjani.

Wachezaji wengi hawana sifa ya kucheza simba ila kwa kuwa ndio waliopo inabidi kwenda nao hivyo hivyo.
Mfumo wa kuingia nao ni 4:3:3 ili kuwarazimisha washambuliaji wa Simba kuanza kukabia juu.
Kikosi cha kuanza ni;
1. Ayubu
2. Kapombe. 4. Che Malone. 5. Inonga 3. M. Hussein

7. Kanoute 6. Mzamiru 8. Ngoma

10. Miquson 9. Kibu D 11. Chama

Hicho ndicho kikosi ningekuwa kocha ningekianzisha dhidi ya mtani tarehe 20/4.
Saido na Barbacar Sarr sio wakuanza hiyo mechi maana ni wazito sana kwenye kufanya maamuzi ya haraka, changamoto hiyo pia anayo Fabrice Ngoma ila ndo hivyo tena hatuna kikosi kipana.
Hao viungo watatu (Mzamiru, Ngoma na Kanoute) lazima waanze wote na wacheze wote katika ili kupunguza risk ya mabeki wetu kifikiwa mara kwa mara.
Miquesson lazima aanze hiyo mechi kwa sababu yeye ni mwepesi kurudi nyuma (katikati) na kutengeneza nafasi za kufunga kwa mshambuliaji no. 9.
Kwa leo ni hayo tu.
 
Ningekua kiongozi pale simba dirisha dogo ningewachukua
Elvis rupia, marouf tchakei, jackson kagoma, bruno gomez, yanick bangala na nikamrudisha babu onyango halafu ningewatoa
Aubin kramo, luis miquisonne, essomba onana, sadio kanoute na saidoo ntibanzokiza

Trust me CAF tusingepigwa nje ndani, FA tusingetolewa na ubingwa tungeendelea kuufukuzia
 
Mtajua hamjui, utopolo. This time around lazma tuwafunge midomo. Mdharau mwiba mguu huota tende.
 
Ningekua kiongozi pale simba dirisha dogo ningewachukua
Elvis rupia, marouf tchakei, jackson kagoma, bruno gomez, yanick bangala na nikamrudisha babu onyango halafu ningewatoa
Aubin kramo, luis miquisonne, essomba onana, sadio kanoute na saidoo ntibanzokiza

Trust me CAF tusingepigwa nje ndani, FA tusingetolewa na ubingwa tungeendelea kuufukuzia
Ila onana na kanoute bado mali hizo. Sema mfumo tu ndo unawafanya wasiwike.
 
Aisee miqueson bado yupo fit sema kocha haanzi nae tu
Ningekua kiongozi pale simba dirisha dogo ningewachukua
Elvis rupia, marouf tchakei, jackson kagoma, bruno gomez, yanick bangala na nikamrudisha babu onyango halafu ningewatoa
Aubin kramo, luis miquisonne, essomba onana, sadio kanoute na saidoo ntibanzokiza

Trust me CAF tusingepigwa nje ndani, FA tusingetolewa na ubingwa tungeendelea kuufukuzia
 
Safari hii simba mkipata hata sare tu, basi nitaamini kweli uchawi upo.
 
Back
Top Bottom