Ili kuepuka migogoro isiyo ya Lazima! Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni muhimu..

Ili kuepuka migogoro isiyo ya Lazima! Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni muhimu..

Hii serikali ya sasa tu ni ya umoja wa Kitaifa, CHADEMA waliamua kuacha kuhamasisha wananchi kusimamia utekelezaji wa maamuzi waliyoyafanya kwenye sanduku la kura mwaka 2010 na kuiacha serikali hii iendelee kuongoza japo uongozi wake ulipatikana kwa uchakachuaji wa matokeo ya urais wa hali ya juu kabisa.

Maamuzi haya yalifanyika kwa sababu CHADEMA na DR Slaa kwao utaifa uko mbele zaidi ya kitu kingine, sasa sielewi unataka serikali ya umoja wa kitaifa ya namna gani? au wewe umoja mpaka watu wagawane vyeo?
 
..."serikali ya umoja wa kitaifa" ndio kichaka mmejipanga kujifichia!?...kweli mmeishiwa mbinu!...
 
Hii serikali ya sasa tu ni ya umoja wa Kitaifa, CHADEMA waliamua kuacha kuhamasisha wananchi kusimamia utekelezaji wa maamuzi waliyoyafanya kwenye sanduku la kura mwaka 2010 na kuiacha serikali hii iendelee kuongoza japo uongozi wake ulipatikana kwa uchakachuaji wa matokeo ya urais wa hali ya juu kabisa.

Maamuzi haya yalifanyika kwa sababu CHADEMA na DR Slaa kwao utaifa uko mbele zaidi ya kitu kingine, sasa sielewi unataka serikali ya umoja wa kitaifa ya namna gani? au wewe umoja mpaka watu wagawane vyeo?

Kwenye maamuzi ndiyo penye maana!!
hayo wanayoyafanya ni mbwembwe tu..
no one cares, what if slaa angekuwa ndiyo prime-minister? ingefaa zaidi
 
mawaziri wao ni Mdee,Wenje,Sugu,Nassari,Lema. Waziri mkuu Dj, hii itakua serikali au bongo movie?
 
CCM itatawala milele bana. Hawa wengine ni waganga njaa tu.
 
Ili kukwamisha hayo mauwaji ni bora sasa kuwashirikisha hata hiyo 2015 katika kuunda serikali..
Usipoikubali serikali ya umoja wa kitaifa ni dhahiri huitakii mema nchi yako..

Na unafurahishwa na wanayofanya CCM..kama ulivyoorodhesha hapo juu

Demokrasia haimaanishi viongozi wote wazuri lazima waunde serikali, bali wawepo wazuri zaidi wanaoikosoa. SUK ni mbinu ya mbaya iliyobuniwa ya kufunika kasoro/uozo. Mara nyingi ni makubaliano ya watawala yasiyo na maslahi kwa wenye nchi.
Kumdhibiti anaechochoea uharibifu ili aunde SUK; ndio njia sahihi ya kuitakia mema nchi.
tragedy of the commons
 
Serikali ya umoja wa kitaifa inaundwa na vyama vyenye itikadi zinazofanana,na zenye mwelekeo mmoja.Tanzania vyama vyetu havina mwelekeo mmoja katika maswali muhimu ya kitaifa kama vile amani,umoja,muungano,siasa na uchumi,haki za binadamu,uwajibikaji.Kila kimoja kinayatazama maswala haya katika kona tofauti.Hata siku moja hatuwezi kupata serikali ya umoja wa kitaifa.Zanzibar iliwezekana kwasababu vyama vikubwa vile viwili vilikuwa vina mwelekeo unaofanana.Hata hivyo serikali ya umoja wa kitaifa iiltokana na mazungumzo wa mwafaka baina ya vyam hivyo viwili,na si vyama vyote.
 
mawaziri wao ni Mdee,Wenje,Sugu,Nassari,Lema. Waziri mkuu Dj, hii itakua serikali au bongo movie?
watanzania ni kweli tunahitaji mabadiliko ya uongozi na ccm imeshapoteza dira na imani ya wananchi wengi......lakini watanzania si wendawazimu hatutakabidhi NCHI kwa genge hili tunahitaji watu smart.....sio blaah blah kutafuta umaarufu tu. tunahitaji watu wenye ababu na msimamo unao fahamika..sio bongo movie.
 
na ndiyo mustakabali wa amani yetu...

...ndugu yangu Sandeni "amani ni tunda la haki"...msitarajie nchi hii kuendelea kuwa na amani kama hakutakuwa na haki...dhuruma na ufedhuli mnaowafanyia wananchi leo mkitegemee kesho mje na hicho kitu mnachoita "serikali ya umoja wa kitaifa" iwe suluhisho ni kujidangaya...suluhisho la kudumisha amani ya kweli ya nchi hii ni moja tu "haki",hayo mengine ni ujanja ujanja ambao hauna nafasi katika kizazi hiki cha digitali..."MWOOGOPENI MUNGU ILI IWAWIE RAISI KUTENDA HAKI"...
 
Last edited by a moderator:
Kwanini tuwe na mashaka na wasiwasi,
Ambao sisi wenye tunaweza kujiepusha nao?

Ni wakati muafaka sasa vyama vya siasa kujiandaa na serikali ya umoja wa kitaifa!

Ni muhimu sana, coz in both political parties kuna viongozi wazuri sana..

CCM tunaviongozi wazuri, mf. Mwakyembe, Sitta, Magufuli and alike! hawa hata kama upinzani utachukua nchi bado kuna haja ya kuwajumuisha katika muundo wa serikali

Wapinzani peke yao hawataweza kuunda serikali yenye mashiko..

Napigia debe serikali ya umoja wa kitaifa, kwa mustakabali wa amani ya Tanzania!!
cc,
majebere, Ritz, chama, HAMY-D
Mbona CCM ilifanya maandalizi ya serikali kama ya Kenya Tangu mwaka 2010 ,ili ikitokea Chama kingine kikachukua nchi masilahi ya mafisadi wa CCM yasiteteleke.
 
Mbona CCM ilifanya maandalizi ya serikali kama ya Kenya Tangu mwaka 2010 ,ili ikitokea Chama kingine kikachukua nchi masilahi ya mafisadi wa CCM yasiteteleke.

there U SEE MY POINT....
 
Back
Top Bottom