Ili kuepuka uharibifu wa nyumba/jengo na kupunguza gharama kwa wapangaji

Ili kuepuka uharibifu wa nyumba/jengo na kupunguza gharama kwa wapangaji

Joined
Dec 30, 2010
Posts
79
Reaction score
55
Hii inawahusu wenye nyumba za kupangisha ama majengo ya biashara ( kupangisha kama Office n.k )
Kwenye swala la Visimbuzi, achana na kufunga dish nyingi kwenye nyumba/jengo moja, ambapo kunakuwa na uharibifu mkubwa wa jengo kutokana na kila fundi ana ufundi wake! badala yake ifungwe dish moja tu itakayobeba visimbuzi vyote vilivyopo kwenye hilo jengo, mf:

Kwenye hiyo nyumba kuna watumiaji wa visimbuzi vya azam 6, badala ya kufunga dish 6 kila kisimbuzi na dish lake, inafungwa dish moja tu, ambayo cable zitaenda kwenye visimbuzi vyote 6. Mwenye nyumba utaokoa uharibifu wa jengo lako na kwa wapangaji pia mtapata unafuu wa kufanya repair pindi itakaposumbua.. Kama gharama ya kumlipa fundi ni Tsh 30,000 itagawanywa kwa watu 6, kila mmoja atalipia Tsh 5,000 hivyo itakuwa umeokoa Tsh 25,000.
Kama mpangaji mshauri mwenye nyumba n kama mwenye mwenye nyumba fanya maamuzi wakati ni huu!!
WhatsApp +255755949413
 

Attachments

  • PSX_20250124_171544.png
    PSX_20250124_171544.png
    1.9 MB · Views: 48
  • PSX_20250124_171453.png
    PSX_20250124_171453.png
    1.9 MB · Views: 42
Hii inawezekana ni sawa ila ubaya ni kuwa Kuna channel za vertical na horizontal , yule aliye kwenye main switch akihamisha channel huwa inavuruga ,mawimbi ya kwenye LNB hii nime experience kwenye lnb za KU BAND
Ikiwa unatumia LNB pekee ama LNB + splitter!?
 
Vipi kama nyumbani kwangu nina tumia DSTV na AZAM,inawezekana kutumia dish moja kwa namna hiyo?
Zinafungwa dish mbili, azam na dstv..
Hii inasaidia kuondoa wingi wa dish kama watumiaji wa azam wapo zaidi ya mmoja na dstv zaidi ya mmoja, lakini si kwa visimbuzi aina mbili tofauti kwa dish 1, mfano wa kawaida tu Dstv degrees 36 na azamtv degrees 7 HAVIHUSIANI.
 
Back
Top Bottom