Ili kuhalalisha usumbufu: Baada ya kuitwa kwenye ajira, unasubirishwa kwa kwa takriban mwezi ili vyeti vihakikiwe, bila kuwezeshwa kujikimu!!

Ili kuhalalisha usumbufu: Baada ya kuitwa kwenye ajira, unasubirishwa kwa kwa takriban mwezi ili vyeti vihakikiwe, bila kuwezeshwa kujikimu!!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Huwezi kuamini kuwa watu wenye akili zao timamu walioaminiwa na Taifa kushughulikia ajira, wakaamua kuweka utaratibu usio rafiki wa kuajiri kwanza kabla ya kujiridhisha na uhalali wa vyeti vya waajiriwa. Halafu akiisha kuitwa kwenye kituo chake cha kazi, ndipo huambiwa subiri kwanza uhakiki wa vyeti vyako ndipo ajira iwe rasmi! Mbaya zaidi wakati mtu amesafiri kwa gharama zake hadi kituo alichopangiwa, huambiwa asubiri (kwa gjharama zake tena) ili vyeti vihakikiwe. Uzoefu umeonesha kuwa zoezi hili la kuhakiki vyeti huchukua kati ya wiki mbili na miezi miwili!! Muda wote huu mwajiriwa mpya hujigharimia mwenyewe kituoni kwake bila msaada wowote na wengine wanaoweza huamua kurudi nyumbani. Tatizo huambiwi usubiri kwa siku ngapi!

Tunajiuliza kwa nini zoezi la kuhakiki vyeti lisingekuwa linafanyika kabla ya mtu kuitwa kwenye ajira? Maana wakati wa usaili wahusika hutakiwa kuonesha vyeti vyao halisi. Kwa hiyo ingewezekana kutuma namba ya vyeti hivyo kwa mamlaka zinazohusika kwa uhakiki. Hata baada ya uhakiki kukamilika na mhusika kuitwa kuja kuanza kazi, bado pesa za kujikimu hapewi nkwa wakati. Kuna kijana sasa ni wiki ya pili tangu aitwe bado hajapewa posho ya kujikimu. Yaani ana wiki 4 toka aripoti (wiki 2 za kusubiri uhakiki na wiki 2 hadi sasa akisubiri posho ya kujikimu). Wanamtaka tu ahudhurie kazini lakini hakuna ajuaye analalaje na anakulaje!! Tuseme tu kuwa hii haikubaliki japo mnatoa sababu zisizoingia akilini.

Mwanzoni sikujua kama huu utaratibu japo unazungumzwa ndivyo ulivyo hadi nilipoona umewekwa kwenye maandishi na mwajiri fulani:​
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Chuo Kikuu ***** (***) kinapenda kuwataarifu waombaji kazi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 13 na 14 Aprili, 2023 kuwa majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Aidha ajira zao zitakuwa rasmi pale vyeti vyao vitakapohakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika.
Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za ajira kwa kufika Chuo Kikuu ***** (***) tarehe 08, Mei, 2023 kuanzia saa tatu kamili asubuhi wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili ili zihakikiwe kabla ya kupewa barua ya ajira.
 
Kama zoezi la uhalkiki lingekuwa linachukua siku moja au mbili nadhani kusingekuwa na malalamiko makubwa. Lakini zoezi linapochukua wiki 2 hadi miezi 2 (bila kuambiwa usubiri siku ngapi), tena bila kupewa posho yoyote kwa muda wote huo, ni mtu wa ajabu tu atakayeona kuwa utaratibu huo unafaa!!
 
Back
Top Bottom