Kwa sasa Simba haina Mfungaji kabisa.
Ukweli ni kwamba
Kagere
Mugalu wote wamechoka sana,
Wakiwa kwenye 18 wanatembea tu wanasubiri kuletewa mipira ili wao wafunge tu.
Mwingine na Bublish hazimwishi mdomoni anasikilizia utamu wake.
Afadhari na John Bocco kidogo anatafuta mipira anakaba na kushambulia mda flan flan.
Straiker anatakiwa kuwa mwenye damu changa anaweza kutafuta mpira na kusafiri nao huku akipunguza mabeki na kufunga ikiwezekana.
Goli la mwisho la Yanga dhidi ya Polisi kazi aliyofanya Mayele ndio kazi ya Straiker.
Simba hakuna anayeweza kuifanya ile kazi.
Ila tunawashukuru sana wote akina Mugalu na Kagere na John Bocco kwa mchango mkubwa waliouleta Simba hadi ikafika hapo na hasa Terminator Kagere kafanya kazi kubwa ya kukumbukwa.
Bocco naye vilevile alijitahidi katika Kipndi chake.
Mugalu tulipigwa toka awali.
Simba inahitaji Straika kama japo yule Mhango, a.k.a Gabadinyo aliyeifungia Malawi goli la kwanza dhidi ya Moroco Afcoan 2022.
Simba kwa sasa imechoka hoi na inahitaji dam changa. Nasikitika sana akina Ajibu, Ndemla, Edward Christopher, Rashidi Juma pamoja na kulelewa Simba na kuwa na vipaji vikubwa wameshindwa kabisa kuzingatia nidham ya Mpira ili kuboresha viwango vyao na kuisaidia Simba.
Hadi tunakuja kuwategemea akina Sakcho na Morrison
Ni hatari sana kwakweli.