Ili kujenga utamaduni wa kufanyakazi

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Ili kujenga jamii yenye utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii ili kuchangia maendeleo ya taifa hili.

Tunapaswa kupitia mabadiliko kadhaa moja ya mabadiliko hayo kama ushauri au pendekezo langu ni kupitishia sheria ya muda wa kazi kwa wafanyakazi katika taifa hili.

Muda rasmi wa kazi utapaswa kufuata utaratibu wa 996 work culture
"The 996 work culture is a practice in China where employees work from 9 AM to 9 PM, six days a week, for a total of 72 hours per week".


Ni muhimu wananchi wakapata muda mwingi zaidi wa kufanyakazi na kujishughulisha katika ujenzi bora wa taifa.

Utaratibu huu uliopo sasa hauleti chachu zaidi ya maendeleo ya kasi jambo ambalo si zuri kwa kuwa bado tupo nyuma sana.

Kwa kiasi kikubwa utaratibu huu mpya 996 kama pendekezo langu utaleta chachu zaidi ya maendeleo ya kasi.
 
Achana na masuala ya mfumo ambao tayari umeuona kwa watu. Cha kwanza ni kubadili malezi na makuzi ya watoto kwenye familia zetu.

Kama mtoto hafanyi kazi za mikono na za nyumbani basi jua ukubwani uwezekano wa huyo mtoto kuteseka na masuala ya ufanyaji kazi ni mkubwa sana.

Ufanyaji wa kazi ni utamaduni unaokuzwa tangu utotoni sawa na tabia ya usafi na tabia zinginezo. Sio miujiza ya kuiga mifumo ya watu.

Siku hizi kuna watoto ambao hawawezi hata kutembea kwa miguu umbali wa kilomita tatu, na wazazi wanachekelea kabisa wanaona ni ufahari wanasahau mwanadamu timamu lazima ashughulishe viungo vya mwili wake.

Ni swala la muda tu tutaona matokeo makubwa ya huu mfumo wa malezi ya mabasi ya njano. Tusubiri tu.
 
Utamaduni huu ukianza maofisini mwetu ukazoeleka nafikiri ni rahisi zaidi kuingia majumbani mwetu
 
Taifa lishakuwa la wakata mauno

Ova
 
Yani tuache kupiga stori za mpira na mziki tupoteze muda masaa yote hayo kuuchosha mwili na akili
 
Yani tuache kupiga stori za mpira na mziki tupoteze muda masaa yote hayo kuuchosha mwili na akili
Mpira na mziki utakusaidia nini wewe na taifa lako ?
 
Kufanya kazi kunaendana na reward zinazotolewa , mtu ufanye kazi saa mbili asubuhi mpaka saa tatu usiku halafu ulipwe elfu kumi kwa siku na hiyo teni oyaa imejaa masimango na kutishiana kinoma yan ! Yaan masaa kumi ya kazi ni kama umefanya 20 🀣🀣 mnachekesha

Ukitaka kuona watu wanajituma ongeza mkwanja , acha kukata kodi za kijinga ! Mizigo ikifika bandari ipite bila usumbufu !

Watu wanajua kupiga mzigo balaa kulingana na mazingira yaliyotukuza kibongo bongo ! Kwenye pesa watu wanajituma aseee !!
 
Ili kuongeza uzalishaji katika nchi serikali ifunge kampuni za kubet, madanguro, vituo vya manabii uchwara na waganga wa kienyeji na pia iboreshe mfumo wa elimu na iongeze ajira kwa vijana .
 
Unajua kwamba huo mfumo ni illegal?
 
Na pia watu waache kutegemea mishahara yao pekee yani waanzishe hata biashara pembeni zitakazowasaidia. Mfano wafanyakazi wa USAID waliofutwa kazi wanakiona cha myema kuni kama hawakuwekeza frdha zao mahali sahihi.
 
kweli aisee watu wamekuwa wavivu sana na tunako elekea ni kubaya zaidi km3 mtu anaita boda hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…