Ili kumaliza utata tunahitaji Ngumi za Live kati ya Ruge Mutahaba na Francis Siza

Ili kumaliza utata tunahitaji Ngumi za Live kati ya Ruge Mutahaba na Francis Siza

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kama ukiwa makini na mfuatiliaji mzuri sana wa Vyomba vya Habari hasa vya Tanzania na ambavyo kwakweli kwa sasa ndivyo vinafanya vizuri vya Clouds fm na Efm utagundua ya kwamba wanachokifanya sasa siyo tena kutuhabarisha, kutuelemisha na kutuburudisha bali sasa wanafanya ' upashkuna ' na ' majungu ' ndani ya Redio zao kitu ambacho sidhani kama kina afya kwa Sisi ' Walaji ' akina GENTAMYCINE na wengineo.

Hivi sasa kumeanzishwa mtindo mpya uliojaa ' mafumbo ' kutoka pande zote mbili huku Clouds fm wakihanikiza / wakinogesha kwa kusema kamwe Binadamu usiwe kama ' Kaa ' ambaye ana roho ya kwanini ( roho mbaya ) akiona mwenzake anataka kufanikiwa na hili likiwa ni ' dongo ' la moja kwa moja kwa Efm na Efm nao Kitendo bila kuchelewa nao wakajibu mapigo kwa kuja na Kihanikizo / Kinogesho chao kinachosema ' hatupoi kama mchuzi wa Pweza ' ikionekana ni ' dongo ' jibu la moja kwa moja kwa Clouds fm.

Nimekaa, nimetafakari na kujiuliza mambo mengi sana hasa la kwamba ni kwanini hizi Redio mbili shindani sasa zimeamua kujikita zaidi katika ' mipasho ' na siyo kufanya Kazi ambayo pengine walikubaliana na TCRA kuifanya kwa Walaji wao? Clouds fm na Efm wanagombea nini labda ambacho Sisi Watu wa kawaida hatujui? Je ' logically ' na ' professionally ' kabisa haya mafumbo yao na hizi bifu zao zina ' tija ' gani katika Tanzania ya Viwanda ambayo sasa tunaitafuta? Na je nani labda yupo nyuma ya huu ' Upuuzi / Upupu ' wote huu? Na ana faidika na nini labda?

Mwisho kabisa nitamuomba sana Waziri wa Habari na mambo mengine Dkt. Mwakyembe anipe ruhusa tu Mimi GENTAMYCINE niweze kuratibu mpambano wa Ndondi / Ndonga za kweli kweli kabisa kati ya Bosi wa Clouds fm Ruge Mutahaba na Bosi wa Efm Francis Siza na Mimi huyu huyu pia nitakuwa ndiyo Referee ili tumpate Mbabe wa kweli na mshindi wa hapa ndiyo atakuwa mbabe wa kweli wa kuanzia Kimwili na mpaka Kiredio redio ili tumalize utata wote kwani tumechoka sasa kila ukikaa tu mara unasiki sijui ' Usiwe Kaa ' huku napo utasikia sijui ' Hatupoi kama mchuzi wa Pweza '.

Halafu hizi Kauli zenu muwe mnaziangalia sana kwani huku mitaani zimeshawaponza wengi. Mimi binafsi kama Saa 3 tu zilizopita nimetoka kumpa Mtu ' Kipondo ' kitakatifu na kilichotukuka baada kuwa na ubishani fulani wa Kisiasa na Kimpira halafu mwishoni ' akashoboka ' na Mimi kwa kuniita Mimi ' Kaa ' ambapo Mwanamume sikuona haja ya Kumchelewesha na nikakumbuka haraka haraka zile styles za Bondia Tyson za ' upper cut ' na ' jeb in ' na ' jeb out ' ambapo nimezitumia zote hizo na hadi hivi natiririka na naserereka na huu uzi aliyeniita ' Kaa ' yupo theatre Mwananyamala anasubiri matibabu ya Kutukuka na hata Ndugu zake walipomwambia kuwa waje wanikamate ' Jamaa ' pale pale nasikia kawaambia wasithubutu kuja kunikamata kwani kama Yeye nimemjeruhi vile halafu ni Kijana mwenzangu aliyekomaa sasa wao na Uzee / Uhenga wao si kuna uwezekano wakija kunikamata basi leo leo katika Familia yao kukatangazwa ' misiba ' mingi na hatimaye Familia nzima itakula hasara kwa kupoteza Ndugu wengi?

Halafu nimeweza kugundua ya kwamba Mabosi hawa wote Ruge Mutahaba na Francis Siza they're sharing something in common. Naomba niishie hapa tafadhali ila natamani sana ' Uadui ' wao huu huu uhame kutoka kuwa wa Kiredio redio na sasa uwe wa Kikweli kweli ili zipigwe ' ndonga ' za maana hadi mmoja ' afletishwe ' kabisa na heshima iweze kutamalaki / kutawala baina yao.

Nawasilisha.
 
E fm watajisalimisha tu mwisho wa picha...
 
hivi kime wapata nini mpaka kuanza kutangaza habari za Mh. wa Dar? au alisha omba msamaha? kama hakuomba msamaha basi hili litakuwa jibu la kwanini usiwe KAA....
 
Acha watupe raha.... clouds waliamin wao wameishika Tz mpk kukawa mpk na vinega nadhan kuja kwa E -FM itapendeza zaidi
 
E FM naona wamefanikiwa hadi kumng'oa Bashite toka upande wa pili.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwani nini maana ya hiyo misemo??....sisi WANAUME WA MIKOANI hatuelewagi mipasho
 
Hicho cha "they are sharing something in common"nadhani ni wote hawajaoa ila wana watoto.na ni watu wa totoz.
 
Back
Top Bottom