Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Habari Wakuu,
Binafsi naamini moja ya chanzo cha nchi hii kutukukusanya mapato yanayoweza kutufanya tupige hatua kubwa zaidi, ni kuwa na taasisi moja(TRA) iliyokabidhiwa jukumu la kukusanya kodi za aina zote tena kwenye nchi kubwa kama yetu.
Moja ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kuwa na utitiri wa kodi na wakati huo huo, kodi zote hizi zinatakiwa kufuatiliwa na kukusanya na chombo kimoja(TRA), jambo ambalo mimi naamini halijaka vizuri na ni chanzo kimojawapo cha kupoteza mapato.
Kwa target wanazojipangia au wanazopangiwa, TRA wanaweza kujiona wanafanya vizuri na hata kuvuka malengo, lakini kumbe kiuhalisia walipaswa kukusanya zaidi ya hapo .
Kwa mtazamo wangu, ili tuweze kukusanya zaidi na kwa ufanisi,TRA inpaswa ana kuvunjwa au kupunguziwa majukumu kwanini inawezekana imeelmewa na hivyo inashindwa kutekeleza vizuri majukumu yake. Mfano mzuri wa hiki nachosema kinaweza kuwa ni hili swala la kutaka kukusanya kodi za majengo kupitia mifumo ya LUKU.
Tukumbuke hii kodi ya majengo mwanzoni ilikuwa inakusanywa na Halmshauri, ila ikaonekana nazo kama zimeshindwa na jukumu hilo likakabidhiwa TRA na kidogo wao walisifiwa kufanya vizuri katika ukusnyaji wa hii kodi kulinganisha na jinsi Halmshauri zilivyokuwa zinakusanya.
Hapa utaona kuwa Halmshauri teyari zilikuwa na majukumu mengi na zikaongezewa mzigo wa kukusanya kodi, hivyo hazikuweza kufanya vizuri kama ambavyo naamini TRA hii yenye utitiri wa kodi nayo itakuwa haifanyi vizuri kama ingekuwa ina-deal na kodi za aina fulani na aina ya kodi zingine zikakusanywa na chombo tofauti.
Mfano, kodi za majengo,ardhi na matumizi ya ardhi zilitakiwa zikusanywe na chombo maalumu ambacho kingeundwa kusajili na kusimamia majengo na pia kingehusika na kukusanya mapato yatokanayo na kodi za majengo na kodi zote zinazohusiana na aridhi na matumizi ya ardhi.
Hata ile kodi ya mapato yanayotokana na biashara ya nyumba za kupangisha(nafikiri iliwashinda) ilipaswa kukuaanywa na chombo tofauti na si TRA na bila shaka ndio maana hata utekelezaji wake hausikiki.
Unapokuwa na taasisi moja inayodili na mambo machache inakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya vizuri kuliko taasisi moja kuwa na mlolongo wa makumu kama ilivyo kwa TANESCO inayohusika na kuzalisha, kusambaza na kuuza umeme nchi nzima na matokeo yake tunayaona.
Hivyo ,naamini kuna umuhimu wa wataalamu kukaa chini na kuangalia ni aina gani za kodi zinapaswa kuendelea kukusanya na TRA(naamimni wao wanafahamu zaidi ) na aina gain za kodi jukumu la kuzikusanya zifanywe na chombo au vyombo vingine vitavyoundwa mahususi kukusanya na kusimamia ukusanyaji wa hizo kodi.
Faida nyingine ya kuunda taasisi kama hizo ni kutoa ajira ingawa kutakuwa na gharama ila zikiweza kukusanya zaidi kuliko wanavyofanya TRA, basi hiyo itakuwa ni faida zaidi kwa nchi na watu wake.