Ili kupambana na 'CCM Mpya', CHADEMA haina budi kukumbatia Ujamaa

Ili kupambana na 'CCM Mpya', CHADEMA haina budi kukumbatia Ujamaa

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Najua hii mada inaweza kuwashtua wengi, ila nipe muda kidogo nitakuelewesha.

Juzi juzi, nilileta mada iliyokuwa inaongelea ni jinsi gani taifa letu sasa linafuata mkondo wa Kifashisti. Nilijaribu kuelezea kwa uwezo wangu huku nikiambatanisha video kadhaa kutoka kwa Profesa mbobevu wa mambo ya Historia na Siasa.

Baada ya kutafakari na kusoma zaidi kuhusu suala hili, nimegundua haya mambo yametokea sana katika historia. Na kwa sababu yameshatokea na yanajirudia, ni budi kujifunza kutoka katika historia.

CCM Mpya kama chama cha kifashisti, kitakuwa na sifa kuu tatu.

Kwanza, kitakuwa kinahubiri sana Utaifa na Uzalendo kama moshi wa kufunika maovu na udhaifu wao.

Pili, kitawakumbatia matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili nalo limeshafanyika kwa kiwango kikubwa.

Tatu, litaminya uhuru wa maoni na mawazo mbadala kuhusu mustakabali wa nchi. Sifa ya kwanza itatumika sana kufanikisha sifa hii ya tatu. Kila mwenye maoni tofauti na ya watawala atakuwa anashutumiwa kuwa siyo mzalendo, ni mhaini, kibaraka, nk. Tuendako ni kubaya zaidi ya sasa.

Hizi ndiyo zitakuwa 'hallmarks' za CCM Mpya. Nini sasa kifanyike?

Nyakati, ambazo watawala wameshindwa kuzizuia ndizo ambazo zimeilazimisha CCM Mpya kwenda kwenye mlengo huu wa kifashisti. Muda na mazingira ya kisiasa na kijamii yamewalazimu na kuwasukuma huko. Ilikuwa ama chama kife au wakumbatie siasa za kipropaganda, mkono wa chuma na kuwaweka karibu matajiri (kwa kuwarubuni au kwa vitisho).

Uamuzi huu hata hivyo utafanya wasiweze tena kudai wao ni chama cha kijamaa. Unaweza kusema walishautupa Ujamaa toka kitambo, ila mazingira haya mapya yatafuta hadaa zote za Ujamaa katika siasa zao.

Ndiyo maana umeshasikia wameanza kuahidiana mautajiri na ubilionea na ni kweli tutegemee kuchipuka 'wazalendo' mabilionea ambao chanzo kikuu cha utajiri wao kitakuwa ni mahusiano ya kisiasa waliyonayo.

Katika ulingo wa kisiasa, mazingira haya yanaacha 'vacuum' inayohitaji kujazwa. Kuna sauti ambazo zitataka watu wa kuwasemea. Sauti hizo inabidi zihubiri yale ambayo Ujamaa ulijaribu kuyapigania.

Kwa muda sana nimekiona chama cha ACT Wazalendo kama chama cha kimkakati. Naona uwezekano ACT kama chama ambacho kiliandaliwa kuja kuziba mwanya huu kabla 'genuine oppositional figure' hajafanya hivyo.

Niliwahi kusema, uamuzi wa Tundu Lissu katika kampeni za Uchaguzi wa 2020 kumrudia Nyerere na yale aliyohubiri miaka ya 1960's ulikuwa ni uamuzi muhimu sana katika kampeni zile.

Laiti kama uchaguzi ungekuwa wa huru na wa haki, uamuzi ule inawezekana ungekuwa moja ya sababu za matokeo chanya kwa CHADEMA. Lakini wote tunajua nini kilifanyika!

Katika historia, mapambano kati ya Wasoshalisti na Wafashisti huwa ni makali sana. Naona kama tunaelekea huko huko.

Ila hilo litatokea iwapo tu kama kutakuwa na upinzani wa kweli wa kukabiliana na Ufashisti. Mamluki watambulike mapema na watengwe. Pia tafakuri ya nguvu inabidi ifanyike ili mbinu sahihi zitambulike na zitumike.

Kwa mtazamo wangu, Siasa ni Sayansi na Sanaa pia. Ukijipanga vizuri, ukajua mbinu za mpinzani wako na madhaifu yake, na pia ukayatambua ya kwako, unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kupambana. Kwenye hili, historia ni msaada muhimu.
 
Chadema Ujamaa? , wapi na wapi ? Kinacho tufanya wengi kuwepo Chadema ni kuamini ubepari, kumiliki mali nyingi na njia kuu za Uchumi.

Tayari tumewekeza vya kutosha Ujamaa tena wa nini? hahaha MZAHA HUU WA MAISHA.


WENGINE TUWEKE WAZI HATA UZALENDO WETU WA KUTO TAKA NCHI YETU ISIGUSWE KWA NIA YA KUIHARIBU TUKIO TAYARI KWA VYOVYOTE VILE KUIFIA NCHI YETU TANZANIA NI KWA SABABU TUSIPOTEZE MALI ZETU.

KWA ITAKAVYO KUWA , TUTAREKEBISHANA NA CCM KIDOGO KIDOGO , HAWA SISI WETU TUU, MBONA WAZAZI WETU WAFIA CCM NA TUNAISHI NA KUPENDANA NAO.
 
Chadema Ujamaa? , wapi na wapi ? Kinacho tufanya wengi kuwepo Chadema ni kuamini ubepari, kumiliki mali nyingi na njia kuu za Uchumi.

Tayari tumewekeza vya kutosha Ujamaa tena wa nini? hahaha MZAHA HUU WA MAISHA.


WENGINE TUWEKE WAZI HATA UZALENDO WETU WA KUIFIA NCHI YETU TANZANIA NI KWA SABABU TUSIPOTEZE MALI ZETU, KWA ITAKAVYO KUWA , TUTAREKEBISHANA NA CCM KIDOGO KIDOGO , HAWA SISI WETU TUU.

Kwa mfumo wa siasa wa sasa wa CCM Mpya, kwa CHADEMA kuwatetea wafanyabiashara hakutakuwa na faida zozote za kisiasa hata kama sera hizo zina faida kwa wafanyabiashara.

CCM wameshawaweka wafanyabiashara on the tight leash.
 
Kwa mfumo wa siasa wa sasa wa CCM Mpya, kwa CHADEMA kuwatetea wafanyabiashara hakutakuwa na faida zozote za kisiasa hata kama sera hizo zina faida kwa wafanyabiashara.

CCM wameshawaweka wafanyabiashara on the tight leash.
One of a major shortcomings is progressively turning the party from Conservative / Center right Party to Militancy /activism Party. This party is for capitalists.
 
Naona kuna baadhi ya watu wanakomaa tu mara ujamaa mara ubepari wakati hawana uelewa wa kutosha kuhusu hii mifumo miwili ya kiuchumi. kiukweli Tanzania sio uchumi wa ujamaa tena wala haiwezi kuwa hivyo na hata kama kuna kiongozi atakuja na Sera za kijamaa atashindwa vibaya mno kuendesha nchi.

Pengine kuna watu hawajui kuwa hakuna pure capitalist economy hata mataifa ya magharibi yanayojulikana kuwa ni yakibepari bado hayana 100%capitalism system. nchi zote duniani labda tukiiondoa North Korea zinaoperate in between capitalism and socialism. Na hapa ndipo tunapata mixed economy ambayo ina elements za kibepari na kijamaa, tofauti inakuwa ni degree of centralization katika nchi husika, mfano katika nchi za magharibi(USA, Canada,UK, German,france nk) pamoja na nchi nyingine za ulimwengu wa kwanza kama Japan, south Korea, Australia na new zealand zina lowest degree of centralization kwasababu wananchi wanamitaji yakutosha asilimia kubwa ya mambo kama huduma za kijamii, miundombinu, viwanda wamewekeza watu binafsi(raia) wenye pesa zao.

Lakini babo kuna sector nyeti kama aviation, railway&road network, elimu, afya mwekezaji mkuu ni serikali, na hapo ndipo pure capitalism inashindwa kufikiwa. Mfano mwingine ni nchi za nordic(Denmark, Norway & Sweden) wana system ya uchumi ambayo free market kama magharibi lkn wana a bit higher degree of centralization kuliko magharibi, yaani serikali inasimamia ama inaregulate sector zote nyeti kama afya, elimu, makazi, miundombinu, lkn wananchi wanaripa kodi kubwa sana kukava expense katika hizo huduma zinatolewa na serikali.

Aina hii inajulikana kama Liberal economy. Afu kuna hizi nchi zetu ambazo wananchi ni maskini lazima zitegemee asilimia kubwa serikali ifanye, kuanzia viwanda, elimu, afya, miundombinu, usafirishaji nk. Na kwa sababu ya kulinda masilahi ya wananchi maskini serikali inaingilia mara kwa mara kwa kuweka bei elekezi mara hivi na vile ili tu kusaidia wananchi. Na kidogo kidogo zinatransform kwenda kwenye free market economy.
 
Hata huko Ulaya, vyama vyenye mlengo wa Kijamaa vipo hata leo na vinashinda chaguzi za kuongoza nchi zao.

Hata huko Marekani, mgombea kama Bernie Sanders amepata support kubwa.
Social democrats au ujamaa wa kidemocrasia ni tofauti na unaoujua wewe. Kwenye huo sekta binafsi ndiyo zinamiliki njia kuu za uchumi. Huo wako wa Nyerere wa maduka ya ushirika ni wa kinyonyaji.

Usikariri tu kuwa ulaya kuna ujamaa.
 
Naona mzimu wa chadema unawatesa sana vijana wa UVCCM
 
Kuijibu nini hii CCM mpya inayokimbizana na mabox ya kura usiku!! Inayoteka na kuumiza watu...inayojibu hoja kwa vipigo wma kutekana..hii ni ya kuumiza kichwa kuijibu nini?

Sasa we ona majibu yake mwenye hii sakata mpya ya hela za Mabeberu...wenyewe wanauliza zilitumikaje...majibu yake sasa duh!!
 
CCM ilishakufa siku nyingi mzee.
CHADEMA inapambana na
TISS.
WAKURUGENZI.
NEC
POLICE.
JWTZ

JIWE LIKIKATA MOTO CCM NDIO INAZIKWA RASMI.
Kumbe CCM ndo imekufa na siyo chadema!
Akili hizi shida kwelkweli, Bora Mbowe kaamua kujikalia kimya kawaacha nyumbu wavuke mto kwa kukanyagana.
 
Kuijibu nini hii CCM mpya inayokimbizana na mabox ya kura usiku!! Inayoteka na kuumiza watu...inayojibu hoja kwa vipigo wma kutekana..hii ni ya kuumiza kichwa kuijibu nini?

Sasa we ona majibu yake mwenye hii sakata mpya ya hela za Mabeberu...wenyewe wanauliza zilitumikaje...majibu yake sasa duh!!
Naelewa unachomaanisha. Mwisho wa siku, maamuzi lazma yafanywe.

Kukaa pembeni na kuwaachia wafanye watakavyo, kutumia mbinu zilezile ambazo hazijawahi kufanikiwa au kutafuta mbinu mbadala kulingana na mazingira mapya?
 
Social democrats au ujamaa wa kidemocrasia ni tofauti na unaoujua wewe. Kwenye huo sekta binafsi ndiyo zinamiliki njia kuu za uchumi. Huo wako wa Nyerere wa maduka ya ushirika ni wa kinyonyaji.

Usikariri tu kuwa ulaya kuna ujamaa.
Wapi nimeongelea maduka ya ushirika?

Sijui na sidhani kama umesoma na kuelewa mantiki ya hoja yangu.
 
Naona kuna baadhi ya watu wanakomaa tu mara ujamaa mara ubepari wakati hawana uelewa wa kutosha kuhusu hii mifumo miwili ya kiuchumi. kiukweli Tanzania sio uchumi wa ujamaa tena wala haiwezi kuwa hivyo na hata kama kuna kiongozi atakuja na Sera za kijamaa atashindwa vibaya mno kuendesha nchi. Pengine kuna watu hawajui kuwa hakuna pure capitalist economy hata mataifa ya magharibi yanayojulikana kuwa ni yakibepari bado hayana 100%capitalism system. nchi zote duniani labda tukiiondoa North Korea zinaoperate in between capitalism and socialism. Na hapa ndipo tunapata mixed economy ambayo ina elements za kibepari na kijamaa, tofauti inakuwa ni degree of centralization katika nchi husika, mfano katika nchi za magharibi(USA, Canada,UK, German,france nk) pamoja na nchi nyingine za ulimwengu wa kwanza kama Japan, south Korea, Australia na new zealand zina lowest degree of centralization kwasababu wananchi wanamitaji yakutosha asilimia kubwa ya mambo kama huduma za kijamii, miundombinu, viwanda wamewekeza watu binafsi(raia) wenye pesa zao. Lakini babo kuna sector nyeti kama aviation, railway&road network, elimu, afya mwekezaji mkuu ni serikali, na hapo ndipo pure capitalism inashindwa kufikiwa. Mfano mwingine ni nchi za nordic(Denmark, Norway & Sweden) wana system ya uchumi ambayo free market kama magharibi lkn wana a bit higher degree of centralization kuliko magharibi, yaani serikali inasimamia ama inaregulate sector zote nyeti kama afya, elimu, makazi, miundombinu, lkn wananchi wanaripa kodi kubwa sana kukava expense katika hizo huduma zinatolewa na serikali. Aina hii inajulikana kama Liberal economy. Afu kuna hizi nchi zetu ambazo wananchi ni maskini lazima zitegemee asilimia kubwa serikali ifanye, kuanzia viwanda, elimu, afya, miundombinu, usafirishaji nk. Na kwa sababu ya kulinda masilahi ya wananchi maskini serikali inaingilia mara kwa mara kwa kuweka bei elekezi mara hivi na vile ili tu kusaidia wananchi. Na kidogo kidogo zinatransform kwenda kwenye free market economy.

Hayo mambo unayoandika nimeyasoma kitambo sana.

Ninachosema ni kuwa CHADEMA ili iweze kusurvive, inabidi iweze kujitofautisha 'in very clear terms' kisera na kiitikadi dhidi ya CCM.

CCM Mpya imeshaamua matajiri wako upande wao, kwa nguvu au kwa hiari. Hivyo basi, CHADEMA hata ikiwatetea na kutunga sera bora za kuwalenga matajiri, hazitakisaidia chama kwa sasa.
 
Back
Top Bottom