Ili kupunguza foleni na kuongeza ajira, Ofisi za serikali ziwe na nightshift...!


hahahaa hapo sawa kumbe tunazungumzia probability
 
Ni balaa foleni kutoka mayfair mpaka njia panda ya coca masaa mawili foleni haitembei kabisa kama kuna traffic police aje pande hizi yani ni majanga.
 
ABIRIA WAHAHA DAR: Lori laharibika Kimara Mwisho na kufunga barabara usiku huu, foleni sasa yaanzia Ubungo-Kimara. Usafiri tabu, abiria watembea kwa miguu.

"poleni sana walioko barabara! kuna taarifa kuwa foleni kwenye barabara ya Nyerere kutokea mijini, magari hatembei', "hapa juu, ni ujmbe ulionifikia kwa njia ya PUSH-MOBILE, by MCL"
 
Sijui nyinyi wenzangu, ila sisi wahudumu wa afya (madokta, manesi, wafamasia na watu wa maabara) tushazoea hilo jambo kitambo. Shame on you ambao mshaanza kusema ngono zitazidi ilhali wafanyakazi wengi tu wa kazi za usiku hawana mawazo hayo, ingawa kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
 
haaaaa kweli aiseee
 
Nenda kafanye research yako upya, night shift kwa nchi km Tanzania bado sana, challenge kubwa ni usalama hamna, na hata wanavyoingia sasa hv wanakuja asbh wanaondoka jioni kuna ambao wanakuwa hawajafanya kazi yoyote kabisa, si ajabu kuwa huyo mtu anapenda Afanye kazi lkn mpangilio wa ofisi na nature ya kazi anajikuta Hana kazi ya kufanya na anachukua mshahara wa bure, ukiwapa nightshift itabidi ofisi iongeze wafanya kazi Wakati hawahitajiki na vile vile hamna mkurugenzi atakayekuja usiku which means hamna maamuzi yyte kwa mda huo yanaweza kutolewa ikihitajika hivyo!
 
kwa majaribio tuanze na TRA; Wizara ya Fedha; RITA; Ardhi na Uhamiaji; Mahakama ya Ardhi pia iruhusiwe kuingia kwenye mfumo huu.
 
Kitu hicho sio rahisi chini ya ILO convention inayohusu night shift workers.
Ila imefika wakati Serikali, ATE, na TUCTA waweke mfumo wa malipo kwa saa, badala ya kwa meezi. Chini ya mfumo huu mfanyakazi alipwe kwa muda halisi anaotumia kuwepo na kufanya kazi. Ukichelewa kufika kazini sawa lakini utalipwa kuanzia ulipofika na ku-punch in ile time card yako hadi utakapo-punch out. Mwisho wa mwezi unahesabiwa saa ulizofanya kazi katika card yako na kulipwa, zikizidi, ule muda wa ziada utalipwa OT nk.
Mfumo huu unapunguza au kuondoa 'peak hours' asubuhi na jioni. Ukiwahi kuingia utawahi kutoka, na ukichelewa kuingia utachelewa kutoka, hata kama itakuwa usiku hutamlaumu mtu, time card yako ndio utachunga mwenyewe, ili uingize saa 8 zinazotakiwa kwa siku.
Hapo msongamano kwenye mwendokasi na daladala pia utapungua.
Hata mabasi ya mikoani nayo madereva wakilipwa kwa saa hakuna atakae endesha kwa kasi, ukiwahi unalipwa kidogo ukichelewa unalipwa zaidi.
Na sio lazima kwamba wafanyakazi wote waingizwe katika mfumo huu, baadhi ya caders kama wataalamu vyuoni, managers, contract staff nk. wanaweza kubaki kwenye mfumo wa kawaida.
 
uko vizuri
 
Yaani tulipane kwa saa? Hii inawezekana kwa nchi zilizoimara kiuchumj, kwa tz waajiri wengi tutafilisika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…