Kitu hicho sio rahisi chini ya ILO convention inayohusu night shift workers.
Ila imefika wakati Serikali, ATE, na TUCTA waweke mfumo wa malipo kwa saa, badala ya kwa meezi. Chini ya mfumo huu mfanyakazi alipwe kwa muda halisi anaotumia kuwepo na kufanya kazi. Ukichelewa kufika kazini sawa lakini utalipwa kuanzia ulipofika na ku-punch in ile time card yako hadi utakapo-punch out. Mwisho wa mwezi unahesabiwa saa ulizofanya kazi katika card yako na kulipwa, zikizidi, ule muda wa ziada utalipwa OT nk.
Mfumo huu unapunguza au kuondoa 'peak hours' asubuhi na jioni. Ukiwahi kuingia utawahi kutoka, na ukichelewa kuingia utachelewa kutoka, hata kama itakuwa usiku hutamlaumu mtu, time card yako ndio utachunga mwenyewe, ili uingize saa 8 zinazotakiwa kwa siku.
Hapo msongamano kwenye mwendokasi na daladala pia utapungua.
Hata mabasi ya mikoani nayo madereva wakilipwa kwa saa hakuna atakae endesha kwa kasi, ukiwahi unalipwa kidogo ukichelewa unalipwa zaidi.
Na sio lazima kwamba wafanyakazi wote waingizwe katika mfumo huu, baadhi ya caders kama wataalamu vyuoni, managers, contract staff nk. wanaweza kubaki kwenye mfumo wa kawaida.