chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Kiuhalisia, wasaidizi wa Majaji ndio huandika hukumu, mishahara yao midogo, na inabidi waendelee kuishi.
Kuna tetesi kwamba wananchi wamefahamu kwamba hawa ndio huandika hukumu, zikiwemo za kesi za mauaji, na wanaishi mitaani na wananchi wa kawaida. Katika kuishi huko, basi Kuna tetesi kwamba ukitaka kutoboa, kesi yako, waone hao wasaidizi wa Majaji.
Na kutokana na wingi wa mashauri, Majaji Wana mida mchache wa kufanya uchambuzi wa majalada, hivyo wao hujikita kuangalia hukumu iliyokuwa drafted na Msaidizi wa Jaji.
Mahakama Ina mawili, iwalipe vizuri, hasa posho maalum ili waendane na hadhi ya wanayemsaidia, ama laa, mahakama ivunje hako ka tetesi kwa kuondoa wasaidizi hao, ili Majaji wafanye majukumu yao wenyewe, na hivyo inakuwa vigumu "kuingilika" kupitia wasaidizi hao.
Usaidizi wa Jaji wengi huuita kukaa "kijiweni"
Kwa kipindi kirefu Sasa mahakama kuu imekuwa haitoi haki halisi (substantive justice) hata kama inaonekana wazi, moja kati ya sababu ni hiyo, wakiona ushahidi "umebana sana" au hawana muda wa kusoma majalada mengi, mahakama yenyewe, bila kuulizwa au kuombwa na wadaawa, itaanza kufukunyua vikosa vidogo vidogo ili tu kuvuruga kesi.
Mahakama imegeuza mashauri ya wananchi kuwa mahali ya "hotuba na mihadhara" ya kisheria bila kujali mashauri hayo yamebeba haki za wananchi.
Wananchi wanasubiri hukumu kwamba shirika la bima limlipe au ardhi ni ya kwake, inatoka hukumu imejaa mahubiri ya sheria na makosa madogo madogo kabisa ambayo hayagusi haki za msingi