Ili kutumia vyema rasilimali za taifa letu ilipaswa ijengwe Hospitali kubwa Mkuranga kumuenzi Mzee Ally Hassan Mwinyi

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Nimeshangazwa sana na uamuzi wa kumzawadia mzee Ally Mwinyi gari aina ya Mercedes lenye thamani ya mil 450.

Kwani kwa umri wake huyu mzee anahitaji gari kama hilo la nini? Kama magari aliyashayatumia sana tena ya kila namna.

Kwanini ili kuenzi utumishi wake uliotukuka usingejengwa hospitali kubwa huko Mkuranga mkoani Pwani? Na hii ingekuwa ni faida na kumbukumbu kwa taifa letu.

My take: Wasaidizi wa viongozi muwe mnawashauri vizuri kutumia rasilimali za umma.
 
Wewe sema Kweli [emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Milioni 450 [emoji2955][emoji848]
 
Mzee Ali Hassan Mwinyi alizaliwa kata ya Kivule. Kwa sasa ipo Ilala Dar es Salaam. Hii ni kwa mujibu wa kitabu chake kilichozinduliwa hivi majuzi "Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha yangu".

Pamoja na hilo, ujenzi wa kitu chochote usilenge kuenzi watu bali mahitaji halisi ya watu wa eneo husika. Huwezi kuweka lami barabara inayopitisha magari manne kwa siku huku Dar kuna barabara inapitisha magari 500 kwa siku lakini ina mashimo na maporomoko yanayosababisha matumizi ya gharama kubwa kununulia spares ambazo ni fedha zinazoelekezwa nje huko kwa wajapan na wazungu.

Tukiangalia huo mfano wa hospitali, hata ukijenga hospitali kubwa, kama population na income ya watu haviendani na hospitali hiyo, utasababisha hasara kwa nchi na wananchi. Hospitali na huduma zote ni lazima zielekezwe pale penye tija zaidi na pale zinapohitajika zaidi.
 
Compare and contrast
 
Hayo magari yalikua 20 tulioewa zawadi na mfalme wa morocco, Magufuli akayachukua, ndio wamempa mwinyi
 
Tayari Rais A H. Mwinyi alienziwa na Mercedece Benz ya Tshs 450million.
 
Kwani yeye Mwinyi so bado yupo,mwambie akajenge mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…