OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Ni sifa ya kila kiumbe kutaka mtoto aendelee kuwepo haswa inaotokea chagua la mtu anayepaswa kubaki. Hii ndio sababu naona haja ya kuwalinda watoto kwa kuwa wao ni vizazi vijavyo. Watoto wana miaka mingi iliyobaki wao kuwepo kuliko mimi ambaye nakaribia ule wastani wa mtu kuishi duniani
Kutokana na uhalisia uliopo kuwa tunauwezekano wa kuendelea kuishi na #CoronaVirus kwa miaka kadhaa ijayo, ipo haja ya kurekebisha baadhi ya mambo kielimu ili kuwalinda watoto wa shule bila kuathiri haki yao ya kupata elimu kwa kipindi hiki.
Ilishauriwa na serikali kuwa kila mwalimu kuhudumuia wanafunzi 40 lakini ni swala ambalo haliwezekani kwa sasa kwani shule nyingi zina wanafunzi wengi kiasi cha kuweka msongamano darasani, kitu ambacho kinaongeza hatari ya wanafunzi kupata maambukizi.
Huu ugonjwa wa #COVID19 unaua tofauti na mapunye au magonjwa mengine ya ngozi. Hivyo kuna haja ya kupunguza msongamano madarasani kwa kuyatambua mambo yafuatayo:
Kuipa nafasi kubwa TEHAMA. Hii iwe kuwa kwa wanafunzi ambao watakuwa na uwezo wa kuwa na ‘laptops’ na vifaa vingine waruhusiwe kusoma bila kufika kwenye majengo shule ili kupunguza wingi wa wanafunzi shuleni.
‘Home Schooling’ itambulike na kuwekwa rasmi, ni suala ambalo baadhi ya wazazi wanaweza kuwafundisha watoto wao nyumbani na kusajili kituo cha kufanya mitihani kwa ajili ya kupata vyeti. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza idadi ya wanafunzi.
Njia ya ‘Home Schooling’ inahitaji ufuatiliaji wa hali ya juu ili kuepuka tatizo la wazazi kuwanyima watoto elimu kwa kusingizia wanawafundisha nyumbani. Watu watakaoruhusiwa kufanya ‘Home schooling’ kwa watoto wawe ni watu ambao wenyewe wanathibitika kuwa na uwezo wa kuwafundisha watoto, hasa walimu wenyewe.
Kama yote hayo yatashindikana, tunapaswa kuona uwezekezaji unaohitajika ili kufanya kila darasa libaki kuwa na wanafuzi 40 tu! Idadi ambayo inaweza kupunguza hatari ya kuambukizana kwa watoto wa shule.
Signed
OEDIPUS