Ili kuyaona makali ya Simba inabidi iwe inacheza na Dar City kila siku

Ili kuyaona makali ya Simba inabidi iwe inacheza na Dar City kila siku

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Nachelea kusema hii ndo timu inayokwenda kushiriki michuano ya kimataifa na trh 13 inavaana na Asec mimosas, kwa namna Simba inavyocheza kwa sasa inatia huruma kwakweli, aieleweki wanacheza mfumo gani.

Leo wanachezesha kikosi hiki kesho wanachezesha kikosi kingine kwa mfumo huo utapataje first eleven inayoelewana? Striking force ya simba kwa sasa wala aiwezi kuwasumbua mabeki wanaojitambua imekuwa mlenda Sana na inakabika kirahisi sana.

Jana bila penalty ya mchongo mechi ilikuwa ni droo kwakuwa prisons waliziba njia zote na simba wakakosa option wala Plan B ya kutegua mitego ya prison.

Sasa Kama wanapata ushindi wa kuhangaika kwenye uwanja wa taifa mzuri ambao wameuzoea wanapokuwa wamekwenda mikoani tusiwe tunakimbilia kuwalaumu wanapoambulia kichapo kwa sababu awapo vizuri kiufundi otherwise wawe wanakutana na timu kama Dar City.

NB: Huyu chama ni mzigo anapokutana na timu inayokaba, ni slow sana na anaigharimu timu inapokuwa inataka kufanya mashambulizi ya haraka, Rs berkane walikuwa sawa kumuacha asingeweza mpira wa kasi na nguvu wanaocheza Waarabu.
 
Tuachie simba yetu bhana! Simba guvu moya!! Na tuna imani na kocha wetu Pablo kutoka Real Madrid.

Hiyo Asec Mimosa yako ikija tunaipiga mkono! Mugalu, Chama, BM3, MK14, na Bocco lazima watupie kudadek!
 
Back
Top Bottom