Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 35,566
- 104,386
Jana kuna mwamba aliweka tangazo humu kwamba serikali imetoa nafasi zaidi ya elfu 1 za wapishi kwenda Uarabuni. Nikajua tu ni utapeli. Serikali haiwezi fanya ivo. Pia email ya kutuma CV ilikua na domain ya gmail.com namba za simu zilikua private nikahisi ujanja ujanja.
Ila leo nikaingia kwenye website ya serikali, kazi.go.tz cha ajabu na kweli tangazo nikalikuta. Na mengine mengi tu.
Nafasi za kazi za vijana mara 800, au 1,000 mara mia ngapi sijui, kwenda nchi za Kiarabu, au Oman au Qatar.
Zote hazijaandikwa kiprofesheno kabisa, wanakimbilia kuandika mshahara mnono Mil 3+, matibabu bure, nauli, malazi etc ila ata majukumu yako ya kazi hayaandikwi. Just wameandika vigezo viwili tu pale, umri na cheti.
Kwa mtazamo wangu naona serikali isijiingize kwenye huu udalali wa kuwapeleka vijana kwenye hizo “ajira” kwa kutumia hawa madalali ambao wengi wao ni matapeli.
Na pili, tushasikia sifa mbaya sana kwa watu wanaoenda kufanya kazi izo nchi. Ya nini kurisk.
Mtazamo tu.
Na pili, tushasikia sifa mbaya sana kwa watu wanaoenda kufanya kazi izo nchi. Ya nini kurisk.
Mtazamo tu.