SoC04 Ili league yetu ikuwe inahitaji mambo yafuatayo(NBC)

SoC04 Ili league yetu ikuwe inahitaji mambo yafuatayo(NBC)

Tanzania Tuitakayo competition threads

Elipa malipo

Member
Joined
May 27, 2024
Posts
7
Reaction score
4
Moja,bodi ya ligi ya mpira wa miguu nchini (TFF )ihakikishe; Kila shabikin anaipa kipaumbere timu ya mkoa anapoishi. Zaidi ya Simba na yanga mfano, kilichosababisha mpaka ligi ya uingereza kukua ni shabiki kushabikia timu ya eneo anapoishi.mfano, mashabiki wa kutoka jiji la Machester wanashabikia Machester.

Manchester,mashabiki kutoka jiji la Liverpool wanashabikia timu ya Liverpool.Hapa nchini timu zilizopo jiji la Dar es salaam mashabiki washabikie Yanga,Simba na nyingine zilizopo jijini hapo na waliopo Jinini Dodoma washabikie timu ya jijini hapo itwayo Dodoma jiji.Hii itapelekea ligi yetu kuwa na ushindani na uhenda ligi yetu ikawa kati ya ligi ishirini bora duniani au kumi bora kabisa.

Mbili,miundombinu ya viwanja vya kuchezea mpira wa miguu viboreshe;Hii ni pamoja na kufanya kuwa vya kisasa vinavyoendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia,vilivyo funikwa juu kwa ajili ya matumizi bora wakati jua limewaka,vilivyo na taa za kisasa visivyo na mwanga mkali sana wala hafifu.

Tatu, serikali iboreshe miundombinu ya barabara,maji,umeme na mawasiliano mfano, barabara itasaidia mashabiki kufika uwanjani kwa muda muafaka ili kutazama michuano inayoendele.

Sababu ya miundombinu mibovu inapelekea kupunguza mudi au shauku za mashabiki wanaoenda uwanjani kwa ajili ya kuangalua mechi za mipira mbambali mfano, mtu anaenda kuangalua (dabi ya kariako) kwa uwanja wa mkapa mara barabara Ina mabonde si Kila shabiki anafurahia hili wengine hawapendi buguza hizo za barabarani.

Nne,kiasi cha wachezaji bora wanaoenda kucheza ligi nyingine isiwe kubwa;Katika ligi ya uingereza Kuna wachezaji wenye majina makubwa ambao bado wapo hapo uingereza mfano,Halandi anaechezea Mchester city, Rashiford anaechezea Machester United.Hapa Tanzania mchezaji mfano chama anatakiwa kubaki, hii itasaidia ligi yetu kukua. Mwingine ni Aziziki anaechezea Klub ya Yanga.

Tano,zijengee shule au akademi;Hizi zitasaidia kukuza vipaji vya wachezaji tangu wakiwa wadogo.Huu ni msingi bora ambao utakuza vipaji vya wachezaji tangu wakiwa na umri mdogo mfano,akademi ya Azam,Yanga na Simba. Hizi zinasaidia kwa kiasi kikubwa ligi yetu kukua.Nchini uingereza kitu kimojawapi kinachowasaidia ni kukuza vipaji vya wachezaji tangu wakiwa wadogo mfano, Rashiford anaechezea Machester Unite.

Tano,kuwepo kwa wawekezaji mbalimbali;Wanaweza wakawa wa nje au wa ndani,lengo ni kukuza ligi yetu(kuifanya ifike mbali kuliko ilipo). Hii itasaidia virabu vingi kujikwamua kutoka katika hali ya ukata(umasikini).Hii itasaidia vitabu vingi kukua na kujitegemea Pia itapunguza wachezaji kuhama kutoka virabu vingine mfano, Dodoma jiji kwenda Yanga au Simba. Kwa kufanya hivyo ligi yetu itakuwa kubwa.

Sita,bodi ya ligi inatakiwa kuzingatia sheria zisizopendelea wachezaji wa ndani ili kuwepo na usawa na kushawishi wachezaji kutoka ligi nyingine kuja kucheza nchini.

Kwa ujumla watanzania tunatakiwa kuwa wazalendo;Hii itashahawishi wawekezaji wengi kutoka maeneo mbalimbali kuja kuwekeza nchini.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom