M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
Hii kitu inaitwa trade-off.
Ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa kauli nyingi anazotoa Tundu Lissu kila anapopata hadhira, they are retaliatory in nature - yaani ni huwa anajibu mabaya yaliyosemwa juu yake au yaliyotendwa dhidi yake.
Nimuoanavyo Tundu Lissu ni mwanasiana mwenye akili nyingi, muungwana lakini yupo makini katika anayoyasema na kuyafanya. Ni mtu anayependa sana kusukuma mbele ajenda anayoisimamia lakini pale inapobidi kurudi nyuma hatua moja hufanya hivyo pia - yaani ni msikivu na anashaurika. Sifa muhimu sana hizi kwa kiongozi awaye yote.
Kwa hiyo yakitokea yafuatayo, ninaamini Lissu anaweza kubadili tone ya hotuba zake:
1. Jeshi la Polisi likiri kwamba halijatekeleza wajibu wake sawasawa katika upepelezi wa watu waliofanya jaribio la kumuua Tundu Lissu mwaka 2017 na muhimu zaidi IGP atoe public statement kwamba sasa wameamua kulivalia njuga tukio hilo. Kwenye intervention hii ya polisi, weledi si tu usemwe kinywani bali uonekane publicly ukitekelezwa kwa vitendo
2. Kwa uzito ule ule ambao vyombo vya habari kama Kwanza TV, Tanzania Daima, nk vimeshushiwa rungu na TCRA, vijarida vyote vinavyomkashifu Tundu Lissu (mfano nimeambatanisha hapa chini) vifutiwe leseni na pia video clips zenye kashfa dhidi yake zinazosambazwa mtandaoni wahusika wake wote wadhibitiwe na kuchukuliwa hatua.
It's as simple as that. Nipe nikupe. You can't eat the cake and have it.
Vinginevyo, mamlaka ikibeza ushauri huu then itakosa uhalali (legitimacy) wa kumwonya Tundu Lissu (or even Zitto Kabwe for tha matter) dhidi ya kutumia lugha ya ukali kwenye hotuba zake - na sisi sympathisers wake (ambao tumo wana CCM na wapinzani wengi) tutaendelea kumchukulia Tundu Lissu kuwa ni victim wa uonevu wa makusudi kutoka kwenye mamlaka ambazo kama zingetekeleza wajibu wake sawasawa kusingekuwa na mtanziko tulio nao sasa.