Ili mwananchi wa kawaida (asiye na simu janja) atumie Mtandao anahitaji Tsh. 272,000 kununua Simu na GB 3. Pato la Mtanzania ni Tsh. 254,000

Ili mwananchi wa kawaida (asiye na simu janja) atumie Mtandao anahitaji Tsh. 272,000 kununua Simu na GB 3. Pato la Mtanzania ni Tsh. 254,000

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
Idadi ya kadi za simu zilizo sajiliwa kufikia 2023
TZ (TCRA)
2020 51.2 million
2021 54.0 million
2022 60.2 million
2023 67.0 million

KE(CA)
2020 57.0 million
2021 60.1 million
2022 63.3 million
2023 66.1 million

UG(UCC)
2020 29.1 million
2021 30.2 million
2022 31.5 million
2023 32.8 million

Gharama za kutumia internet
Tanzania
Kwa wastani wa kipato cha 253,000 Tsh kwa mwezi, ili Mtanzania awezekutumia mtandao
Anahitaji kununua kifaa amabacho bei ya chini kwa wastani ni 150,000 - 300,000 TSh (108.7% ya kipato chote)
Wastani wa bei ya internet kupitia kifurushi ni 1600-1800Tsh kwa 1 GB na kila mteja alitumia wastani wa MB 3,714 ambayo inagharimu kati ya 5,808 TSh and 6,534 TSh
Sawa na 2.44% wastani wa kipato cha Mtanzania.
108.7+2.44)= 111.1% ya wastani wa kipato cha mtanzania ndio kinahitajika katika mwezi wake kwanza mtandaoni

Kenya
Kwa wastani wa kipato cha 454,000 Tsh kwa mwezi, ili Mkenya awezekutumia mtandao
Anahitaji kununua kifaa amabacho bei ya chini kwa wastani ni 250,000 - 370,000 TSh (68.3% ya kipato chote cha mwezi)
Wastani wa bei ya internet kupitia kifurushi ni 1,600-2,800 Tsh kwa 1 GB na kila mteja alitumia wastani wa MB 3072 ambayo inagharimu kati ya 4,770 TSh and 8,340 TSh
Sawa na 1.97% wastani wa kipato cha Mkenya.
68.3+1.97)= 69.9% ya wastani wa kipato cha Mkenya ndio kinahitajika katika mwezi wake kwanza mtandaoni

Uganda
Kwa wastani wa kipato cha 259,000 Tsh kwa mwezi, ili Mganda awezekutumia mtandao
Anahitaji kununua kifaa amabacho bei ya chini kwa wastani ni 130,000 - 269,000 TSh (77.05% ya kipato chote cha mwezi).

Wastani wa bei ya internet kupitia kifurushi ni 1200-2440 Tsh kwa 1 GB na kila mteja alitumia wastani wa MB 5222 ambayo inagharimu kati ya 6,050 TSh and 12,000 TSh
Sawa na 3.48% wastani wa kipato cha Mganda. (77.05+3.44)= 80.5% ya wastani wa kipato cha Mganda ndio kinahitajika katika mwezi wake kwanza mtandaoni


Kulingana na Takwimu za world bank za 2021, kwa nchi zinazoendelea angalau mtu anapaswa kupata wastani wa 6GB kwa mwezi. Mtanzania anahitaji kuongeza matumizi yake sasa kwa 39.5% ili kufikia viwango vya world bank vya wastani wa matumizi ya mtandao yanayochukuliwa kama ni ya wastani kwa nchi zinazoendelea.

Mkenya anahitaji kuongeza matumizi yake sasa kwa 50% ili kufikia viwango vya world bank vya wastani wa matumizi ya mtandao yanayochukuliwa kama ni ya wastani kwa nchi zinazoendelea.

Mganda anahitaji kuongeza matumizi yake sasa kwa 14.9% ili kufikia viwango vya world bank vya wastani wa matumizi ya mtandao yanayochukuliwa kama ni ya wastani kwa nchi zinazoendelea.

Mbadala wa kuchagua mtandao mwengine ili kupunguza mzigo wa gharama za kuwa mtandaoni

Tanzania
31% Vodacom
28% Airtel
27% Tigo
12% Halotel
2% TTCL
Licha ya Mtanzania kuwa na zaidi ya Watoahuduma watano wa kuchagua, nchini Tanzania kuna beielekezi ya gharama za mtandaoni hivyo kuhama mtandao haimaanishi kutapunguza gharama za kukaa mtandaon. Wastani wa mtandaoni kwa watoa huduma wote ni Tsh 2.1 kwa MB.

Ulinganisho wa kupenya kwa mtandao katika nchi tatu za Afrika Mashariki hadi kufikia 2023

Tanzania
Kupenya kwa Mtandao: Takriban 53.5% ya watu
Watumiaji wa Mtandao: Zaidi ya watu milioni 33.1.

Kenya
Kupenya kwa Mtandao: Karibu 32.7% ya watu
Watumiaji wa Mtandao: Takriban watu milioni 17.9.

Uganda
Kupenya kwa Mtandao: Takriban 24.6% ya watu
Watumiaji wa Mtandao: Takriban watu milioni 23.7
 
Tz wengi wanaishi kwa ujanja ujanja, utakuta mtu hajui hata kusoma lakini anatumia simu janja naye aonekane mjanja, mwingne utakuta hana kazi maalumu lakini ana miliki simu janja na kiswaswadu
 
Simu janja hata elfu 60 unapata kitaani. Bado tunatumia la elon musk
 
Back
Top Bottom