Ili nchi inufaike na rasilimali zake lazima iwe sehemu ya supply chain na sio kutegemea kodi na share tu

Ili nchi inufaike na rasilimali zake lazima iwe sehemu ya supply chain na sio kutegemea kodi na share tu

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
5,559
Reaction score
8,747
Jaribio la kutaka kumpa mwekezaji hiyo supply chain yote kwa mda wa miaka 20 au 30 sio sawa hata kidogo kwa nchi kusubiria miaka 30 ya mwekezaji ndo uanze kunufaika moja kwa moja na rasilimali zako- narudia tena sipingi waekezaji ila ni muhimu nchi kuwa sehemu ya supply chain ya rasilimali ilizokuwa nazo ndo sababu ya gulf countries kuendelea sababu rasilimali zao kama gesi na mafuta wao ni sehemu ya supply chain

Mfano Supply chain ya gesi asilia ni kama ifuatayo
  1. Drilling
  2. Pipeline transporting
  3. Refining
  4. Industrial use
  5. Domestic use

Nikiwa Rais wa Tanzania miradi ya offshore drilling na pipeline itafanywa na serikali ili kama nchi iweze kunufaika kwa wigo mpana zaidi ya kutegemea tu kodi na share tu

Kutokuwa sehemu ya supply chain ndo moja ya sababu kule kanda ya ziwa kuwa na migodi mingi lakina kuna umaskini wa kutisha kwa sababu sisi kama nchi hatuko sehemu ya supply chain ya uchimbaji wa dhahabu

Serikali itajenga
  1. Offshore drilling
  2. Pipeline yenye millimetres 32 na 47

Note; Ikishajengwa hizo offshore drilling na pipeline ceo, na wafanyakazi wengine wanaweza ajiriwa hata foreigner kikubwa wawe na ufanisi na kufikia Target walizoekea sio lazima waajiriwe watanzania

Waekezaji watawekeza kwenye
  1. Refining
  2. Secondary industries such as automotive,
  3. Small factory

Katika mambo ntakayoyafanya ni kujenga offshore drilling wako watu wanaotumia nguvu kubwa sana kuaminisha watu kwamba hatuwezi bila waekezaji huu ni mpango wa kuhakikisha hatunafaiki na rasilimali zetu, ni kweli ni gharama ila kama nchi inawezekana

Hilo swala la tusubirie miaka 30 au 20 ndo tunufaike na rasilimali siafiki nalo hata kidogo

Tutajenga world-class offshore drilling na onshore drilling kwenye vitalu vyote vya gesi ambavyo vipo Tanzania hatutahitaji ruhusa au kibali kutoka kwa mtu yeyote yule namimi naamini tunaweza

Mradi mwingine ni kujenga pipeline ambazo zitakuwa za aina mbili
kwanza ni kutoka kwenye offshore na onshore drilling na itakuwa na ukubwa wa millimetres 32.

Pili ni kutoka kwenye vituo vya kuhifadhia gesi ilivovunwa kutoka kwenye offshore drilling na onshore drilling mpaka mikoa tofauti tofauti hili bomba litakuwa linabeba gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya viwandani na majumbani na lilakuwa na ukubwa wa millimetres 47

viwanda kama vya smelter, refining vitakua na direct access ya gesi hii ambayo haijashafishwa ambayo inafaa kutumika viwandani kama mbadala wa umeme wa Tanzania ambao ni mdogo na hauwezi kuhudumia smelter na refining
 
Back
Top Bottom