Ili niweze kufanya kazi TTCL natakiwa nisomee masomo gani na kozi gani chuoni?

Ili niweze kufanya kazi TTCL natakiwa nisomee masomo gani na kozi gani chuoni?

guwe_la_manga

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
2,820
Reaction score
2,758
Miye ni muhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012 kwa masomo ya HGL, ningependa kupata mwongozo wa nini nifanye.

Je, HGL yangu ya div 2 inatosha?

Au kuna somo inabidi niyareseat?

Na kama kwa HGL inawezekana ni chuo kipi kinatoa masomo hayo kwa ngazi ya diploma?
 
Kwanza hongera mdogo wangu kwa hatua uliyofikia.

Pili ndoto ya kufanya Kazi TTCL bado ni ndogo. Fikiria mashirika makubwa na makampuni ya Kimataifa na uhakika utafika tu kukupenda,
HGL ukitaka kufanya kaz mashirika makubwa soma.

Marketing, Human Rssources, Sociology, na Business Administration.

Changamoto ni kwamba ushindani ni mkubwa sana ila sio kwamba haiwezekani.

Mungu akutangulie
 
Fani nyingi tuu unaweza kusoma na kufanya kazi pale, mfano kuna Telecom, Electrical, Information Technology, Computer Engoneering, Computer Science, Law, na nyingine nyingi
 
Somea fani yeyote ila nzuri ni Telecommunication Engineering, Marketing, Accounting ila hakikisha una mjomba yeyote pale katika kiti cha Mkurugenzi au maswahiba zake na atokee Usukumani.

Otherwise usipoteze muda hata ku apply!
 
Kasomee kati ya hizi; sheria, uongozi wa biashara, masoko, mawasiliano ya umma, uajiri watu.
Au tafuta aina ya mafunzo yenye mchanganyiko wa yote hayo.
 
Back
Top Bottom