Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua.
Kwenye principle ya uchaguaji wa jambo flani katika mengi, maana yake umekubali kuyakosa hayo mengine. Kumbuka kuwa haimanishi hayo mengine huyahitaji ila imekubidi kuchagua jambo moja muhimu zaidi kwa wakati huo.
Ukiangalia kwa umakini, utagundua Serikali inafanya vitu vingi sana. Inatumia fedha nyingi sana kutekeleza mambo ambayo ni muhimu kwa ustawi wa jamii yetu.
Hata hivyo, ukiangalai mambo yanayofanyika, utagundua hakuna impact kubwa katika mambo hayo. Utakuta mambo mengi yamefanyika ila ni nusu nusu, au yakiwa na mapungufu mengi. Kwa ufupi tukiulizana ni jambo lipi tunaweza sema kama Taifa tumefanikiwa angalau kwa 90% bila shaka tutahangaika sana kulipata jambo hilo.
Pamoja na Serikali kujinasibu kutumia Matirioni ya fedha tangu tumejitawa kutoka mikononi mwa Wakoloni, lakini hebu angalia uhalisia ulioko kwenye jamii;
i) Mpaka sasa bado kuna uhaba wa matundu ya vyoo kwa watoto huko mashuleni
ii) Mpaka sasa kuna uhaba wa vyumba vya madarasa, hakuna maabara za kisasa za kufundishia, hakuna vitendea kazi vingine muhimu na bado kuna watoto katika nchi hii bado wanakaa chini kwa kukosa madawati au viti vya kukalia.
iii) Katika sekta ya Afya bado kuna changamoto ya wataalamu, vifaa Tiba n.k
iv) Mpaka sasa kuna watu wanakunywa maji kutoka mabwawani na wapo wanaosubiri maji usiku wa manane wapate angalau ndoo 2 za kutumia.
v) Mpaka sasa hatuna hata Highway moja yenye umbali hata km 100 ambazo zimejengwa kisasa, namanisha Highway yenye lanes nyingi ambazo magari hayakutani (One way road traffic), na madaraja ya kisasa.
vi) Achana na kukosekana kwa umeme vijijini, eti mpaka sasa kuna vijiji havina mawasiliano kwa njia ya simu, yaani ni mpaka wapande juu ya miti kupata mawasiliano.
vii) Na mengine mengi.......
Nini kifanyike?
Tuachane na kisingizio kuwa nchi hii ni kubwa sana na mambo ni mengi sana. Tuache kisingizio kuwa watu wanazaliwa wengi kila siku, hivyo pamoja na jitihada za Serikali kujenga vyumba vya madarasa, hupelekea Serikali kuelemewa na mzigo mkubwa..
Tufanye hivi...
Kama nilivyogusia hapo, tujaribu ku-focus katika jambo moja na kulipa kipaumbele kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko mengine kwa muda flani.
Namanisha nini? Simanishi kuwa tujikite kwenye jambo moja pekee na kuacha mengine, la hasha. Simanishi kuwa tujikite kwenye elimu pekee na kuacha watu wakifariki kwa kukosa matibabu..
Isipokuwa namanisha kuwa;
Badala ya kuhangaika na miradi mingi kwa wakati mmoja na kutumia pesa nyingi ambazo impact yake kitaifa inakuwa ndogo, tuweke Mpango Mkakati wa Kitaifa utakaowezesha ku-maintain huduma muhimu zilizopo isipokuwa miradi mipya ifanyike kwa jambo moja pekee tutakalolipa kipaumbele zaidi.
Kwa mfano: Tunaweza kuhakikisha tunatumia fedha za kuhudumia sekta nyingine ili kuwezesha maisha yaendelee kama kawaida, ila tukaelekeza fedha nyingi zaidi za miradi katika sekta moja pekee kwa muda wa mwaka 1 au miaka 2.
Namanisha tunaweza kuipa sekta ya Elimu kuhakikisha kuwa tuna madarasa ya kutosha, walimu wa kutosha, maabara za kisasa, maktaba bora, madawati ya kutosha. Kunakuwepo na miundombinu mingine bora kwa kila shule ya Msingi, kila shule ya Sekondari ya Kata na nyinginezo kwa muda wa miaka 2.
Tukimaliza hapo tunahakikisha kuwa kila mtaa/kitongoji, kila kijiji/ kila kata ina maji safi na salama.
Baadae tunahamia kwenye Umeme, barabara, n.k.
Hakika baada ya miaka 20 tutakuwa na mambo yakujivunia na tunakuwa TAIFA lililopiga hatua kubwa sana.
Karibuni kuboresha wazo..