Ili TAKUKURU iwe na meno ishirikishwe katika mipango ya idara na mashirika ya umma

kuna tuhuma nyingi sana kwamba takukuru pia ni wala rushwa. hapo unasemaje?
 
kuna tuhuma nyingi sana kwamba takukuru pia ni wala rushwa. hapo unasemaje?
Inawezekana ni kweli kwa kuwa wengi wa vigogo wa TAKUKURU wametokea polisi ambako rushwa inanuka! Hivyo kuna kila sababu kuiangalia upya taasisi hii!
 
Inawezekana ni kweli kwa kuwa wengi wa vigogo wa TAKUKURU wametokea polisi ambako rushwa inanuka! Hivyo kuna kila sababu kuiangalia upya taasisi hii!
sio kweli, wapo ambao hawajawahi kufanya polisi. wanachokifanya na ambacho kinasemwa, wakiamua kukuchunguza wanakuja na kajalada na kukutonya halafu wewe utajiongeza. ukieleweka yameisha usipoeleweka lazima uburuzwe mahakamani tena kwenye kesi ambayo hata hawatashinda.
 
Binafsi nimehojiwa mara mbili nikiwa Rukwa na Mtwara lakini kwa kuwa sikuwa na tatizo lo lote katika utendaji wangu sikuwahofia. Wao walikuwa ama wanapewa taarifa zisizo sahihi au walikuwa wanabumba hoja wenyewe ambazo ni za uongo na vitisho kwangu lakini sikuwajali kwa kuwa nilijua niko safi! Pale Mtwara waliacha kunibugudhi baada ya kwenda kumuona kamanda wao wa mkoa.

Kwa kifupi wapo ambao wana tabia za hovyo ambao ukiwaendekeza watakuharibia kazi!
 
wadau ningependa kujua ,kwenye kaz za takukuru kuna form ambayo muombaji hutakiwa kujaza nakukusanya sasa kuna swali huwa wanauliza kama umeoa/kuolewa. je kazi yao kama umeoa watakupokea kwel?
 
wadau ningependa kujua ,kwenye kaz za takukuru kuna form ambayo muombaji hutakiwa kujaza nakukusanya sasa kuna swali huwa wanauliza kama umeoa/kuolewa. je kazi yao kama umeoa watakupokea kwel?
Ndiyo utapokelewa na kuajiriwa! Taarifa hizo ni muhimu ili kama kuna cho chote mfano uhamisho mwenza wako na watoto kama wapo wapewe stahili zao kama nauli nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…