Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
1. Katiba Mpya - Lazima itungwe katiba mpya yenye meno inayoweka hatua anazopaswa kuchukuliwa kiongozi endapo ataivunja. Katiba hii iweke misingi ifuatayo;
a) Rais ateue Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mawaziri tu- Akishateua lazima hao watu wathibitishwe na Bunge. Mawaziri wasiwe Wabunge
b) Majaji waombe kazi na kufanyiwa usahili kwenye public hearing na wanaofuzu ndo wateuliwe na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Walindwe kweli na Katiba iliyo na meno.
c) Mikoa itambulike kama Kanda za kiuchumi na Wakuu wa Mikoa waombe kazi na kufanyiwa usahili unaofanyika kwa Public Hearing. Majukumu yao yawe kusimamia masuala ya kiuchumi katika mikoa
hiyo. RAS ndo wasimamie masuala yote ya Mikoa na wawe watumishi wa Umma wanaopangiwa kazi na Katibu Mkuu Kiongozi
d) Nafasi za Wakuu wa Mashirika ya Umma zisiwe za kuteuliwa. Watu waombe hizo kazi na wachujwe kwa kufanyiwa usahili. Wawajibike kwa Bodi zao na sio Wanasiasa.
e) Nafasi za DAS, DED zote ziwe ndani ya Utumishi wa Umma. Asipewe nafasi hizo nje ya Utumishi wa Umma. Na watumishi wa Umma waombe hizo nafasi na kufanyiwa usahili. Wawe na Kinga ya kutoingiliwa na mtu yeyote katika maamuzi ikiwemo wanasiasa.
f) Bunge- Kigezo cha kuwa Mbunge kiwe Elimu ya Chuo Kikuu
g) Siasa na Utendaji- Watendaji walindwe kikatiba dhidi ya Wanasiasa.
Tukifanikiwa kuwa na Katiba mpya na tukaweka haya tumetoboa