Mr Excel
JF-Expert Member
- Jul 31, 2021
- 526
- 1,675
Kalamu ya uandishi wangu inakusanya maono ya fikra, hisia, mawazo na shauku ya msomaji mwenye ari ya kutaka kufahamu kichwa cha makala hii kinalenga nini hasa? na je, makala hii inanigusa? na itaniletea mabadiliko baada ya kuisoma na kuielewa vizuri?. Bila shaka na hofu ondoa ndugu msomaji wa makala hii ukweli ni kwamba makala hii inatoa jibu la NDIYO kwa mabadiliko yako na kugusa nyanja zako upande wa kiuchumi, jamii, siasa, tamaduni, imani na suala zima la ajira bila kusahau uwezo mkubwa wa kupanga mipango yako na kuikamilisha ndani ya muda muwafaka.
Naanza kutuma yangu makala kwa mfumo wa barua kwako mpendwa msomaji uliyesubiri muda mrefu maarifa, mbinu na ujuzi wa kukutoa hapo ulipo.
Salamu kwako msomaji, Tushajihishane kufahamu Mwangaza ni nini? japo sio neno geni kulisikia katika masikio yako.
Mwangaza-Hii ni hali ya kitendo kwa mtu kupambaukiwa kifikra yaani kupata ufahamu wa wapi ulipotoka, unavipaji gani, udhaifu gani, upo wapi, unazungukwa na nani, una mikakati gani, na unaelekea wapi kwa muda gani utakuwa umeshafikia mikakati yako.
Nyenzo, Naam bila shaka tuliweza kujifunza shule ya msingi kuhusu nyenzo hivyo ufahamu tunao kuhusu hili neno. Kwa lugha ya kigeni wanaita "material" hapa bila kuchanganya na lile neno "resources" lenye maana ya rasilimali. Neno Nyenzo lina maana ya kila kitu kinachokuzunguka na una uwezo wa kukipata kwa uchache au wingi kisha kuweza kutumia katika kurahisisha kukamilika kwa hitajio lako. Kuna msemo unasema "ukitaka kuwasha mshumaa ni lazima uunguze njiti ya kiberiti kwenye kasha lake" Maana yake ni nini tukihusianisha na kichwa cha makala hii pamoja na Uhalisia wa maisha yetu"
Dhumuni la makala hii ni kukukumbusha Ndugu msomaji kwamba: Ukitaka kutimiza malengo yako yawe makubwa au madogo ni lazima ukubali kupambania ndoto zako, ni lazima utumie muda vipaji na hata pesa zako ili kupata unachohitaji. Maisha hayajawahi kuwa rahisi na hayatakuwa rahisi, maisha hayategemei uwepo wa bahati ila maisha yanaandamana na bahati zilizokuja kwa juhudi na jitihada zilizofanyika nyuma ya pazia ambazo kwa macho ya nje Leo tunasema unabahati umefanikiwa haraka sana bila kuumia au kuhangaika. Vijana wanalalamika kwamba Fulani amewekwa katika nafasi Fulani sababu ana juana na mtu Fulani! lahasha! haipo hivyo kwa sababu nyuma ya pazia ni kweli amewekwa kwenye hiyo nafasi ila alikubali kuchoma nyenzo zake na ikampelekea yeye kuonekana anafaa katika hiyo nafasi japo kwa sura ya nje tunaona amependelewa bila ya kuwa na kipaji cha hali ya juu kama chako.
Usinukuu vibaya au kuingiza mitazamo hasi, soma tena na fikiri kiundani zaidi nyenzo muda, kipaji, juhudi, nidhamu na mwisho pesa katika kulipia gharama ya kujifunza kile kilicho ndoto ya maisha yako.
Niazime sikio kijana, Maisha ya karne hii ya 21 imetawaliwa kwa teknolojia zenye utaalamu na wataalamu wabobezi. Dunia ya sasa inahitaji watu wenye nyenzo zaidi ya moja yaani uwe na ujuzi zaidi ya mmoja, kumbuka pia kwamba kipaji pekee hakitoshi bila ya kuwa na nyenzo zingine kama zile za nyenzo watu, ujuzi mtaji, nyenzo kuu ya mawasiliano, nyenzo ya jitihada na uvumilivu katika safari yako ya mafanikio.
Vijana tumekuwa na tabia ya kuwa walalamikaji, wapanga mipango na wakosoaji katika mitazamo hasi. Dunia ya sasa inahitaji Vijana wenye uwezo wa kuwa watafuta majibu, watatua matatizo, wanaovumilia changamoto kwa kuambatana na utatuzi yakinifu, wenye kuanzisha mambo na kutimiza mipango kwa asilimia mia. Naomba tufikiri wote kwa pamoja Hivi mtu akiwa anakulilia shida kila siku, anakuletea malalamiko bila kutafuta suluhisho, je unafikiri huyu mtu utamfikiriaje?? Naam, hivyo unavyomfikiria hasi, mvivu na asiyewajibika ndivyo hivyo wanakufikiria ambao unawapelekea shida na malalamiko yako kila siku ili tu uonewe huruma. Hapana kataa hii hali na kubali kutumia nguvu zako, Fanya biashara, jitume kiutafutaji, jiajiri kwa biashara ndogo ndogo na Weka aibu pembeni jenga tabia ya kuanza na kuthamini kilicho kidogo sasa ili kiwe kikubwa hapo baadae.
Mwisho wa makala hii natuma barua yangu hii kwa Vijana wote ulimwenguni, wazee, wanawake na wanaume ziwafikie zangu salamu na hitimisho la kukumbusha kwamba:- Kuanzia sasa ondoa hofu, ondoa aibu, kata mizizi ya uvivu na kuahirisha mambo, acha kukesha mitandaoni bila ya dhumuni maalumu, acha tabia zenye kutumia nguvu zako vibaya, afya yako na Mali zako.
Muda wote kuwa imara kiafya, kiakili na kihisia, Waza mawazo chanya, panga mikakati mikubwa, inenee maneno mazito kwamba kuanzia Leo unaenda kupata Mwangaza wa kubadili maisha yako na kutimiza mikakati yako kwa nguvu zako na akili zako kabla mwaka haujaisha. Ahsante kwa Kusoma makala hii nakutakia kila raheli katika hatua zako za kutumia nyenzo zako ili kufikia mwangaza.
Wako Mtiifu,
Mr.Excel
Piga kura, sambaza makala hii na weka maoni yako ili andiko hili likalete mabadiliko kwa wote.

Upvote
5