Mafiningo
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 4,435
- 4,662
Hakika kila mbabe ana mwamba wake, hivi ninavyoandika hii Dk 45 za first half zimemalizika na kwa kweli Azam ndio waliokuwa juu kwa kila kitu na kila idara.

Kumbe Yanga ni timu mbovu kiasi hiki?

Kama Azam wangekuwa makini mpaka dk hii wangekuwa wako mbele kwa mabao matano, ngoja tuendelee kuangalia .

Kamusoko hoi kwa Salum Abubakar!

Yanga imekubali kipigo cha magoli manne bila majibu kutoka kwa Azam FC mjini Zanzibar katika michuano ya mapinduzi inayoendelea ikiwa ni kipigo chake cha kwanza tangu michuano hio ianze.

Sasa Yanga itasubiri mshindi kati ya Simba na Jang'ombe boys ambao watacheza kesho jioni.

USHAURI - YANGA IJITOE KWENYE MICHUANO HII ILI KULINDA HESHIMA YAKE , SIKU IKIKUTANA NA MNYAMA WATAADHIRIKA ZAIDI , HERI LAWAMA KULIKO FEDHEHA .