Ilikuaje Sudan Kaskazini ikawa na watu wenye rangi nyeupe (Waarabu) na Kusini kukawa na watu weusi?

Ilikuaje Sudan Kaskazini ikawa na watu wenye rangi nyeupe (Waarabu) na Kusini kukawa na watu weusi?

Mkuu mada hii umeiandika kwa dhana.

Picha ya rais aliyepinduliwa Omar al Bashiri ni mweupe yule?

Je baraza linaloongoza serikali ya mpito umeona picha zao ni weupe wale?

Weusi na majiyakunde kama wasomali utasemaje weupe pee!
mkuu unaona hao wanafanana na wasudan kusini?
 
Sudan ilikuwa ni nchi moja kabla ya kugawanyika na kuwa nchi mbili hivi karibuni. Sasa binafsi nashangazwa kidogo kwa namna hii nchi ilivokuwa yaani kule kaskazini raia wa kule ni weupe peee mpaka nywele zao ambazo ni ndefu kama waarabu halafu wa kusini ni weusi tiiii nadhani Afrika nzima ndio wanaongoza kwa weusi.

Ilikuaje ikawa hivi?

Au wale wa kaskazini ni walowezi? Maana hawafanani hata kidogo japo ilikuwa nchi moja.

Mkuu sababu ya uwepo wa watu wa asili ya waarabu na weusi kuwa pamoja NI sawa na zile zilizowafanya ndugu zetu wa Zanzibar kuwa na watu weupe na weusi huku ikionekana kutoka nje kuwa weupe ni wengi.

Mambo ya kiutawala na biashara Kama yalomfanya Sultan kuhamia Zanzibar kutimiza maslahi yake hivyo kupelekea kuchangamana kwa jamii tofauti.

Ila kilichopelekea jamii hizi kuangukia ndani ya nchi moja nini u mkutano wa kidhalimu wa Berlin wa mwaka 1884 walipoligawa bara la Afrika.

Lakini Sudan ilikua chini ya Misri huku Misri yenyewe ikiwa chini ya Uingereza. Wakati huu ni wazi waarabu toka Uarabuni kupitia Misri na Wamisri wenyewe walihamia Sudan kwa Mambo mbalimbali iwe biashara au utawala ila katika ukaaji wao walijipata wakichangamana na wenyeji ambao ni Wanubia ambao ni weusi tii. Mchangamano huu ndio umeleta matokeo haya tuyaonayo Leo Kuona Watu wa Asili ya Kiarabu wakiwa kaskazini karibu na mpaka wa Misri na weusi wakiwa hasa maeneo ya kusini.

Mgawanyiko zaidi wa Sudan ukaleta kuundwa kwa taifa jipya la Sudan kusini na Moja ya sababu ya mgawanyiko huu ni tofauti ya kidini na kikabila, watu weusi waliona kama wenzao wenye Asili ya Kiarabu wanawatawala na kuwaonea hivyo wakadai kupata Taifa lao ambalo watajitawala.
 
south sudan hawa weusi?

Ndio hiyo na wanaongea kiarabu vizuri tu. wako wanasoma vyuo Misri na wamejaa tu mi nilivyowaona ikabidi niulize wenyeji ndio wakanijibu kuwa before wakoloni waje ilikuwa nchi moja
 
Ndio hiyo na wanaongea kiarabu vizuri tu. wako wanasoma vyuo Misri na wamejaa tu mi nilivyowaona ikabidi niulize wenyeji ndio wakanijibu kuwa before wakoloni waje ilikuwa nchi moja

Navyojua south ni wakristo na hawaongei kiarabu, halafu washamba washamba na sio wastaarabu kabisa wale jamaa.
 
Navyojua south ni wakristo na hawaongei kiarabu, halafu washamba washamba na sio wastaarabu kabisa wale jamaa.

Basi hawa ninaowaona hapa ni wale South Sudanese waliotokea north wanaongea kiarabu fluent na kanisani tuna sali nao tena wao ndio wanajaza kanisa wako wengi sana
 
Sudan ilikuwa ni nchi moja kabla ya kugawanyika na kuwa nchi mbili hivi karibuni. Sasa binafsi nashangazwa kidogo kwa namna hii nchi ilivokuwa yaani kule kaskazini raia wa kule ni weupe peee mpaka nywele zao ambazo ni ndefu kama waarabu halafu wa kusini ni weusi tiiii nadhani Afrika nzima ndio wanaongoza kwa weusi.

Ilikuaje ikawa hivi?

Au wale wa kaskazini ni walowezi? Maana hawafanani hata kidogo japo ilikuwa nchi moja.
Nadhan ni mambo ya utumwa! Pengine kuna watumwa walichukiliwa Ugandan miaka ming iliyopita wakapelekwa huko kufanyishwa kazi, then wakazaana. Hata hivyo waarabu wa Sudan kaskazin sio kiviiiile....Ni kama waarabu wale wa nzega na bukene tuuu
 
Kweli unaakili wewe! Umejuaje hao ni wahamiaji tu? Na wametokea wapi? We unafikiri ardhi hii ya kwetu sisi tu, weupe hawana haki ya kuishi!! Unachekesha sana 😁😁😁

Kama ni wahamiaji basi hata kiarabu wanachoongea kingefanana na gulf countries people Mf Emirates, oman, Qatar, saudia n.k. ingawa wanaongea kiarabu na wanaelewana vizuri tu na mataifa hayo lakini kuna baadhi ya maneno wanatofautiana japo wote ni waarabu.
Wewe unaonekana akili yako haipo poa, umekurupuka😬.
Nimekwambia asili ya bara la Afrika ni Jamii ya watu weusi hao waarabu ni wahamiaji tu, hujaelewa nn hapo? Kwani muarabu wa Afrika kutofautiana lugha kidogo na waarabu wa Asia unaona nalo ni ajabu? Mbona hata blacks hatuongei lugha moja? Waarabu wote Afrika ni wahamiaji toka Asia.
 
Huenda wapo wanaoongea kiarabu lakini ni wachache sana
Kama ilikuwa ni nchi moja na lugha ya taifa ni Arabic basi wale South Sudanese walioenda shule wanaongea kiarabu wale ambao hawajenda shule hawaijui ni kama Kenya wale ambao hawajasoma hawajui English or Swahili lakini huwezi sema Kenya hawajui English na Kiswahili kwa sababu ya hiyo percent mdogo ya illiterate
 
Sudan lugha yao ya taifa ni kiarabu, ni kama saudia, emirates na oman. Hata kama hujaenda shule kiarabu utajifunzia kwa wazazi n.k maana ndio lugha mama.

Hao south sudan sina hakika kama ni wazawa ama wahamiaji kutoka sehemu zingine.
 
Kumbuka kabla ya South Sudan kujitenga walikuwa nchi moja ya Sudan na lugha ilikuwa ni kiarabu kwa hiyo kama unazingumzia watoto wa ki South Sudan waliozaliwa miaka 9 iliyopita baada ya kujitenga basi hao hawajui kiarabu
 
Back
Top Bottom