Ilikuwa Safari Ndefu

Ilikuwa Safari Ndefu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ILIKUWA SAFARI NDEFU

Ilikuwa siku kama ya leo sasa imetimu mwaka mmoja.

Picha hizo hapo chini ni maofisa kutoka Heritage Centre for Liberation of Afrca na TBC wakiwa Ukumbi wa Arnautoglo kunirekodi kipindi kinachohusu uchaguzi wa TAA mwaka 1953.

Wanaogombea nafasi ya Rais wa TAA ni kijana wa mjini miaka 30, Market Master wa Soko la Kariakoo na pia Kaimu Rais wa TAA na Katibu, Abdulwahid Kleist Sykes mtoto wa mfanyabishara maarufu Dar-es-Salaam Kleist Abdallah Sykes.

Anaejaribu kuchukua nafasi hiyo ni Julius Kambarage Nyerere miaka 32 mtoto wa Chief Burito Nyerere kutoka Butiama, msomi kutoka Chuo Kikuu Cha Edinburgh, Scotland na mwalimu wa shule ambae hakuwa anafahamika na wengi Dar-es-Salaam.

TBC na Heritage Centre for Liberation of Afrca walikuwa wanatengeneza vipindi 52 kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere na uhuru wa Tanganyika.

Vipindi hivi 52 vitarushwa kimoja kila siku kwa mwaka mzima kila juma kipindi kimoja.

Walitaka nieleze historia ya uchaguzi huu nikiwa kwenye ukumbi wa Arnautoglo wenyewe mahali ambapo uchaguzi ulifanyika miaka 70 iloyopita.

Historia hii haikupata kuelezwa popote ila ndani ya kitabu alichoandika Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," na kuchapwa London mwaka wa 1965.

Mwalimu mwenyewe hajapata kueleza historia hii lau kama ni muhimu mno katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Siku hii ndiyo siku Mwalimu alipoanza safari yake ndefu ya siasa.

Kinachoshangaza ni kuwa historia hii haijapewa umuhimu unaostahili.

Picha ya tatu ni Asha Hajji wa TBC akinihoji kuhusu siku ile.

Picha ya nne inamuonyesha Mwalimu Nyerere siku za mwanzo akiwa na wana TANU wenzake, Mama Maria, Bibi Titi Mohamed, Rashid Mfaume Kawawa na wazalendo wengine.
 
Back
Top Bottom