Simphola
Member
- Jan 9, 2014
- 84
- 19
Mazingira yepi Simphola? Sio Zanzibar, Huku jua lilichomoza zamani, Walipiga kura mara tatu 1961, 1963, kuchaguwa chama gani kiwaongoze baada ya uhuru wa 10th December 1963, kwa hamasa kubwa. Washindwe kujibu kura ya maoni? Dont ridicule us.
Hizo kura za vyama unafikiri zingefanya nini bila John Okello kujitoa mhanga? Nachosema hapa ni kuwa, mchakato wa katiba kupitia wananchi huchukua muda mrefu, na dhamira ya wakati ule ilikuwa kuungana mapema ili kujenga umoja wa kiafrika, sawa na maazimio ya 1963, unajua kuwa muungano huu ulikuwa ni kwa shinikizo na maslahi ya nani? Unataka kusema katiba mpya ijayo itakuwa haina mapungufu? Unakumbuka ni mapendekezo mangapi yalikataliwa na Karume? Unakumbuka public opinion ya watanzania 1965 iliyofanywa na gazeti la uingereza ili reveal nini juu ya muungano?