Ilikuwa tarehe kama ya leo january 2011

Ilikuwa tarehe kama ya leo january 2011

Hongera sana siri kubwa ya wewe kutofika kijiji cha mateso cha mjini BAN ni uvumilivu wako na busara ulizo nazo happy birthday marejesho mungu akupe miaka mingine mingi hapa jf.

asante sana Slave . Huwa nikiona matusi kwenye uzi najitahidi kuhama haraka nisikwazike..Pili kitu kama sina ushahidi nacho,najaribu kutokukisema......
namuomba Mungu azidi kuniongezea uvumilivu......
 
Last edited by a moderator:
Happy birthday jf marejesho...
Ila ujumbe kuhusu mume wako umenitachi sana.
Naomba nikupe list kwenye upinzani Paloma kaongezeka tena your hubby Filipo kamuambia amemkatia fast jet aje a town asuke yeboyebo na amnunulie white dresss.
Pia kuna Lusile japo kaja kivingine mumeo nae anazengea...
Pole shostito

Asante amu . Nashukuru kwa taarifa za kiinteligensia....Huyu mume mwaka ukianza anakuwa kama anakaugonjwa fulani ka kupenda na kupendwa...Ni mapungufu aliyonayo ambayo nayaelewa fika..Siwezi kumuacha kwa hilo ila nashirikiana nae bega kwa bega ili siku moja yeye mwenyewe aseme basi..... Paloma na Lusile welcome onboard.......
 
Last edited by a moderator:
Huyu pendapenda Filipo nimemngoja nadhani ananiwekea naiti tu. Mamito! shostito! shem! marejesho hongera mpenzi kwa kutoboa miaka bee tangu utie guu humu. Najua ushakutana na changamoto nyingi sana humu ndani na zimekukomaza! Endelea kuelimisha!
 
Last edited by a moderator:
Tarehe kama ya leo, mwezi wa kwanza, mwaka 2011 (6th Jan 2011), Nilipata fursa ya kujiunga na Jamii Forums. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kudumu humu jamvini mpaka sasa ..

SABABU YA KUJIUNGA
Habari za SIASA motomoto nilizokuwa nikizipata miaka ile kwenye JAMBO FORUMS, ndizo zilikuwa chachu ya mimi kujiunga tena...

KWA NINI TENA?
Baada ya kukaa nje ya mtandao kwa muda mrefu, nadhani Jambo Forums waliondoka na password yangu... Nilijaribu sana kukumbuka password lakini niliambulia patupu...."Sikuwahi kupata wazo la kuwauliza Mods"

MAFANIKIO
Nimeweza kupata marafiki wengi ,ambao tunafurahi pamoja, tunashirikiana katika mambo mbalimbali.Kimsingi wamekuwa ni sehemu ya familia yangu....
Lini ningekwenda Tanga na kuenjoy kiviile kama sio JF? Big Up sana Arusha-WING, TA-WING na DAR-WING....

Nimeweza kufuatilia mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea Nchini,ya kupendeza,kuhuzunisha nk.... Daima nitashukuru kuwepo kwa Jukwaa la Siasa maana bila wao, hakika nisingefika hata huku Chit Chat....

SHUKRANI ZA PEKEE.

Ziwafikie Mods ambao mpaka sasa hawajawahi kunipa hifadhi kule BAN GUEST HOUSE... Nasikia kule kuna mateso balaa, alinidokeza Mungi . Muendelee na moyo huo huo, mkizidi kufanya kazi yenu kwa umakini, msinikumbuke kabisa katika huo ufalme wa BAN..

Pili kwa mume mpenzi Filipo ,kwa kunidaka juu juu.. Nakiri kwamba upinzani upo ,tena mkubwa toka kwa Smile , ladyfurahia , sweetlady Arabela amu ila sintolala usingizi kabisa.... Baadhi ya niliowataja kwa namna moja wanampenda au wanapendwa na mume wangu.... Nayahesabu kwamba ni mapungufu ya kibinadamu....
UJUMBE:
Mimi na Filipo hatukukutana barabarani ,na kama hamuamini angalieni lini tulijiunga JF....


Nawatakia Upendo, Furaha , na Mafanikio katika kila Jambo mtakalolipanga kwa mwaka huu mpya 2013...

Copy: PakaJimmy , Blaki Womani , Preta , Lily Flower , Arushaone , Mr Rocky , Mungi , Mzee wa Rula , LiverpoolFC , Erickb52 , Smile , Arabela , Dark City , madame V , Nicas Mtei na wengine ambao sijawataja...

Hongera sana Mama totoo! Tulijiunga siku moja kwa malengo mamoja na hatujawahi kupigwa ban! Na hatutarajii kuipata!
Jipambe utoke bomba nikupeleke Sundown Cannivo mpz! Me love you much!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom