Ilikuwaje Azam wakaenda kujenga uwanja Chamazi? Tunalitia taifa aibu

Ilikuwaje Azam wakaenda kujenga uwanja Chamazi? Tunalitia taifa aibu

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Wakuu sio kwa ubaya ila kiukweli nilikua sijawahi kufika chamazi na nilikua na picha nzuri tu kichwani ya maeneo ya huko. Sasa majuzi nikajikuta nimefika kutokana na shughuli zangu kunipeleka huko.

Kiukweli nilijiuliza maswali mengi sana nini kilipelekea Azam kuamua kwenda kujenga uwanja kule ukizingatia kuna michuano ya kimataifa inayofanyikiaga kule na timu mbalimbali toka mataifa ya nje yautumia ule uwanja. Ni aibu kwa mazingira yale kumpeleka mgeni wa aina yoyote aisee hasa njiani mpaka kufika pale ulipo uwanja.

Uwanja wenyewe na mazingira yake ni super ila maeneo yanayozunguka hapo na njia nzima kwakweli ni aibu. Labda uwanja wa KMC pale mwenge utatutoa hii aibu aisee, Chamazi ni sio poa kabisa, maeneo mengine kama Mbezi, Kiluvya hadi kibaha walikosa kabisa? Kigamboni je?

Anyway sitaki kuwakwaza wakazi wa kule ila daaah... Tunajitia aibu hasa kwa wageni, bora mechi zikachezwe hata Zanzibar kuliko Chamazi kuepuka aibu.

Screenshot_20240624-213847.jpg
 
Dah, Kutujumuisha Sote Kwa sentensi Ya ' Tunajitia Aibu' Sio poa kbs...!

Hapo Ungesema 'nimejitia Aibu'... !

Chamazi ilivyo ndo Uhalisia Wetu Maeneo mengi Tanzania.. na Wala Sio Jambo La Kulionea aibu au kufichaficha..!

Sasa pale Jangwani palivyo na Maeneo jirani na Klabu ya Yanga yalivyo unataka kusema Yanga Wanajitia Aibu kuwepo pale..? Acha hizo
 
Shida nini kwamba barabara haipitiki hakuna lami au kuna vita maeneo yale au Pana ubaya gani
 
Una mambo ya kizamani, nyumbani kwako unapaoneaje aibu upatapo wageni? Kama unakuja kwangu we mgeni sitaona aibu kwa mazingira yangu ninapoishi ila siku nyingine ukija tena utakuta kuna mabadiliko makubwa/maendeleo
 
Dah, Kutujumuisha Sote Kwa sentensi Ya ' Tunajitia Aibu' Sio poa kbs...!

Hapo Ungesema 'nimejitia Aibu'... !

Chamazi ilivyo ndo Uhalisia Wetu Maeneo mengi Tanzania.. na Wala Sio Jambo La Kulionea aibu au kufichaficha..!

Sasa pale Jangwani palivyo na Maeneo jirani na Klabu ya Yanga yalivyo unataka kusema Yanga Wanajitia Aibu kuwepo pale..? Acha hizo
Au ile picha waliyoipiga uwanja wa Taifa watu wa Al Ahly kabla ya mechi na Simba ikatrend sana tokana na mazingira na majumba mabovu yanayouzunguka uwanja wa Mkapa. Ule ndio uhalisia wa maisha yetu mkuu na sio aibu. Sisi watanzania tu hohe hahe na maskini.
 
Lile eneo lote pale alipewa bure na serikali.. baada ya kushinda kesi..

Ni kujitanua tu kibiashara kama NATO wanavyo jitanua kuelekea mashariki
 
Back
Top Bottom