Ilikuwaje Samson Akaua Simba?

Ilikuwaje Samson Akaua Simba?

and 100 others

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2023
Posts
3,707
Reaction score
12,367
Hivi zamani middle east kulikuwa na simba?
Ile hadithi ya Samson kutoka kwenye biblia alipomkamata simba kwa mikono akamrarua vipande natafakari wale simba walikuwapo middle east?

Biblia inasema Samson alipokuwa akielekea Timna na wazazi wake kwenda kuonana na yule mwanamke wa kifilisti aliyetaka kumuoa, akakutana na mwana-simba, yule simba akaunguruma akimuungurumia Samson, Samson alimpasua yule simba kama mwana kondoo.

Waamuzi 14:5-6
5 Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia.
6 Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.

Timna ukisoma ulikuwa ni mji wa wafilisti, kiufupi ni middle east ile ile, Timna inasemekana ni karibu na Jerusalem kwa umbali wa miles kama 20.

Nipo natafakari kule jangwani kulikuwa na simba, au abadiliko tabia nchi?

Je? Simba waliwahi kuishi middle east? na kama walikuwepo waliwinda wanyama wapi? swala, pundamilia?
Nini kilipelekea simba wale wakaondoka middle east?

Wajuzi watuelezee.



A005264_Samson-Fighting-a-Lion.jpg


Halafu jamaa alipokuwa anarudi akakuta kwenye ule mzoga wa simba kuna asali na nyuki, jamaa akalina asali yake, akachukua asali akaendelea na safari akilamba asali huku anakwenda :AYOOO::Analyze:

Naendelea nilipoishia Waamuzi ule mlango wa 14 aya ya 5 hadi ya 6, naendelea na 7.

7 Basi akatelemka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana.
8 Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali.
9 Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.
10 Basi babaye akamtelemkia huyo mwanamke; Samsoni naye akafanya karamu huko; kwa kuwa vijana ndivyo walivyokuwa wakifanya.

Ni hayo tu.. :peepoRun: .............. :RUNNING:
 
Luka 17:6

Kwenye masuala ya imani ukishaweka logic unapoteza sifa ya kuwa mwamini.

Ushaambiwa ukiwa na imani unaweza uambia mti mkuyu ng'oka ukajipandikize baharini na mti ukatii. Yaani ukajing'oa zake huoooo mpaka baharini halafu ukajipanda.

Sasa njoo na Logic.
 
Back
Top Bottom