Ilikuwaje ukaibiwa simu??

Uzembeee huu
 
Mteja alikuja dukani duka lilikuwa jipya akawa anaagiza vitu vingi Kwa mkupuo , alikuwa anaagiza vitu vinavyohitaji kupanda na ngazi. Baadae akaghaili kununua hata hivyo vitu. Akawa ameondoka na simu.
Wizi wastaili hii sijui wanapumbaza watu akili!?unakuta anakwambia leta hiki leta kile hata kustuka hamuna
 
Huku ndo kuibiwa sasa..
Wewe sio mzembe ila tu walikubananisha
 
Mwaka 2011 nikiwa na HTC nimeweka mfuko wa shati nikawa nakatiza kariakoo, jamaa akanikanyaga kwa makusudi mguu wa kulia, nilivyogeuka akawa anasema njia tembea kwa tahadhali nikataka nishikane nae huku nikimwambia wewe ndio umenikanyaga tena kwa makusudi.

Nikaona mambo yasiwe mengi niondoke zangu sasa ile nimeingia kwa daladala nitoe simu hakuna kitu ndio hapo nikagundua kumbe ile ilikuwa planned issue ili wkt nabishana nae mtu mwingine upande wa kushoto achomoe simu.
 
Simu 5 nimeibiwa kwa ajili ya ulevi wa bia. Simu 1 tu ndio niliibiwa kawaida niliacha dar nikaenda mkoa mwingine, kuna watu nikawapigia simu wafanye usafi ndio wakasepa na simu nilipoweka.
Nilipowauliza wakasema hawakuiona.
Uzembe
 
Uzembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…