Fundi manyumba
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 3,799
- 8,063
Uzembe ahahahNiliwahi ibiwa simu mara moja tu kwenye maisha yangu yote na haiku ya gharama, tangu kipindi hiko niko makini vibaya mno.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uzembe ahahahNiliwahi ibiwa simu mara moja tu kwenye maisha yangu yote na haiku ya gharama, tangu kipindi hiko niko makini vibaya mno.
Uzembe huuNilikuwa tungi demu akasepa nayo, sikumuona tena mpaka leo. Najua itakuwa ni kopo tu huko alipo maana nimeshaiblock na kila ninapoitafuta online haionekani.
UzembeNimewahi ibiwa simu mara moja Tu.Hii haikuniuma Sana kwasababu ilikua ishajichokea.Niliiacha ofisini nikaenda ofisi zingine narudi simu haipo.
AmbakanjaniHabari zenu
Nimeanzisha huu uzi ili kupata experience ya kutunza simu zetu zisiibiwe, kama umewahi kuibiwa unaweza kutuambia ilikuwaje!
Uzembeee huuMimi sikuibiwa ila nilikaa kwenye gari na dada mmoja mzuriiii, ikabidi nimpe simu aandike namba zake, akaipokea akawa anaandika namba ikatokea dereva kagonga dog, ikawa tafrani pale nikashuka haraka nikapanda gari lingine bila kusahau nimempa simu yule manzi....
Huu uzembeAh mi walikuwa wananiibiaga simu nikiwa nimelewa.. Na wameniibia simu nyingi sana.. Toka nimeacha pombe mwaka wa kumi huu sijaibiwa simu..
Ahahahah uzembe huuMimi niliibiwa simu 2 -
Ikiwa unaishi nyumba za kupanga jitahidi ufunge mlango mchana ndo ulale
Wizi wastaili hii sijui wanapumbaza watu akili!?unakuta anakwambia leta hiki leta kile hata kustuka hamunaMteja alikuja dukani duka lilikuwa jipya akawa anaagiza vitu vingi Kwa mkupuo , alikuwa anaagiza vitu vinavyohitaji kupanda na ngazi. Baadae akaghaili kununua hata hivyo vitu. Akawa ameondoka na simu.
Huku ndo kuibiwa sasa..story za watu zinachekesha mno..!!
simu ya kwanza kupotea, hii nahisi sikuibiwa nilifanya uzembe, nilikuwa nachat kwenye daladala tulikuwa wanachuo wengi tunaenda zetu Coco beach, enzi hizo tunajikuta wajanja balaa, nikawa nachat zangu nairudishia mapajani, muda wa kushuka kwenye daladala nikanyanyuka tu na mkoba wangu shwaaaaaaa, nahisi ilidondoka na zile purukushani sikuhisi chochote..!!
Nafika chini sioni simu na daladala ishayeyaa, ilikuwa bado mpya iliniuma balaa..!!
Simu ya pili, mzee hii nilikabwa Arusha na vibaka,😂😂
Hili tukio huwa linachekesha sana lakini lilinifanya kuwa traumatized vibaya mno, usiombe kubananishwa ukutani na majamaa wawili halafu kuna mvua flani na kigiza giza hivi, na hapo nipo hatua chache mno kufika nyumbani jumlisha nimevaa ki skirt kifupi cha kumwaga, niliwatolea mpaka hela Mimi mwenyewe ili wasije waza vitu vingine, siwezi sahau hii..!!
Simu ya tatu, walaqhi' Mimi nimeshindikana, japo story zote hizi zimetokea miaka mingi mno iliyopita, hii sasa ukiskia uzembe ndiyo huu, hii huwa hata siwaambii watu maana ni aibu, nilitapeliwa hii simu kijinga sana walaqhi', nilikuja kujicheka baadaye kabisa nikajiona bonge moja ya phaller..!!
Simu ya nne, hii ni Ile style ya kupuliziwa dawa ya usingizi dirisha mpaka linafunguliwa hujui, unaamka asubuhi unaskia kichwa kizito balaa, hakuna simu wala pochi yenye Pesa za kazini na miwani ya macho, wale wajinga waliiba mpaka lipstick halafu mkoba wakautupa nje huko, hii ilinikuta nikiwa Tanga, mzee ukiskia kudata ndiyo hii, hii hata sikulia tena, nilihuzunika tu sababu ya Pesa za watu baasii, ila kwenye simu nilikuwa nimeshakuwa gaidi..!!
Simu zote nilizotumia hivi karibuni sasa, it's either nigawe, iharibike yenyewe ama niuze, nimekuja kuwa makini balaa, enweiz, si sana sababu hakuna aijuaye kesho..!!😂😂
UzembeNiliibiwa cm Maramoja tu na niliibiwa na mgonjwa ambaye nilikua namuhudumia
UzembeWiki ilopita tu nilipigwa push kwenye daladala wakati wa kupanda na sim ikapigwa hapohapo nakaa kwenye siti sim sina, dah jasho lilinitoka. Dsm sio
UzembeSimu 5 nimeibiwa kwa ajili ya ulevi wa bia. Simu 1 tu ndio niliibiwa kawaida niliacha dar nikaenda mkoa mwingine, kuna watu nikawapigia simu wafanye usafi ndio wakasepa na simu nilipoweka.
Nilipowauliza wakasema hawakuiona.
UzembeMwaka 2011 nikiwa na HTC nimeweka mfuko wa shati nikawa nakatiza kariakoo, jamaa akanikanyaga kwa makusudi mguu wa kulia, nilivyogeuka akawa anasema njia tembea kwa tahadhali nikataka nishikane nae huku nikimwambia wewe ndio umenikanyaga tena kwa makusudi.
Nikaona mambo yasiwe mengi niondoke zangu sasa ile nimeingia kwa daladala nitoe simu hakuna kitu ndio hapo nikagundua kumbe ile ilikuwa planned issue ili wkt nabishana nae mtu mwingine upande wa kushoto achomoe simu.
UzembeNilimpatia Mtu cm Aongee , Afu Gafla Sikumuona.
Yani Sijui kama bado Anaongea since 2019
UzembeSavei kwa Wizi niliibiwa simu Stationary Savei Darajani ubahili wa kutoa copy vitabu vya tender Tabata nikaona niende Savei bei chee.
Ilikuwa hiviHabari zenu
Nimeanzisha huu uzi ili kupata experience ya kutunza simu zetu zisiibiwe, kama umewahi kuibiwa unaweza kutuambia ilikuwaje!
Nlikua nawai kuubiriUzembeee huu