Ilimwagika damu,itamwagika damu alisikika mkenya mmoja

Ilimwagika damu,itamwagika damu alisikika mkenya mmoja

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Dosari zilezile za uchaguzi uliopita kama hazitafanyiwa kazi mkenya mmoja akasikika akinena damu itamwagika tena
 
Kenya figisu zao wanazifanya kiboya sana wanapaswa waombe msaada kwa chama la wana kupitia kwa Born town.
Ni uzuzu wa Watanzania kukaa kimya kiboya la sivyo kingekuwa kishanuka,hakuna figusi za kisayansi hapa
 
Mbunge wa Kenya ametoweka baada ya kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake Magharibi mwa Kenya.
Walioshuhudia wanadai Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alimpiga mwanamume huyo kichwani wakati wa mabishano katika kituo cha kupigia kura kaunti ya Bungoma.
Polisi sasa wameanzisha msako wa kumtafuta mbunge anayewania muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Wamempa saa 24 kujisalimisha kwa mamlaka zinazochunguza mauaji hayo. Bw Barasa si mgeni katika mabishano.
Mwaka jana, alikamatwa na kushtakiwa kwa kumshambulia mwanamuziki wa nchini humo. Habari zaidi zinasema aliwahi kuhudumu katika jeshi.
 
Born town gani ww, mi mtz, Tz kuna mambo ya kipumbavu Sana na wananchi wengi ni mafisi tu, elimu ndogo ndio maana yanaiba kura na hayataki tume huru.
 
HomeSiasaMaafisa 8 wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya Wakamatwa

Maafisa 8 wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya Wakamatwa​

MAAFISA nane wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC) wamekamatwa na Polisi na kusimamishwa kazi baada ya kukutwa wakifanya mkutano wa siri.

Maafisa hao wamekamatwa katika kaunti za Homabay, Kisumu na Bungoma ambapo walikutwa wakiwa na baadhi ya wagombea wa nafasi tofauti katika Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Agosti 9, 2022.

Maafisa wengine wanne wa tume hiyo ya uchaguzi wamesimamishwa kazi katika maeneo ya Bunge ambayo ni Ndiwa na Webuye Mashariki mwa nchi hiyo.

Maafisa hao wamesimamishwa baada ya kukutwa wakiwa wamekutana kwa siri na wagombea wa kiti cha wawakilishi wa Bunge la kaunti moja nchini humo na wagombea wa Ubunge.

Kwa mujibu wa ushahidi wa video uliotolewa na Polisi unaonyesha kwamba katika mojawapo ya tukio alionekana Naibu Msimamizi wa kituo cha kupigia kura akimshawishi mkubwa wake kukubali kwa lengo la kumsaidia mmoja wa wagombea kupata ushindi.

Baadhi ya maafisa wengine wa tume ya uchaguzi katika kaunti ya Bungoma wametoroka baada ya wenzao kukamatwa nyumbani kwa mmoja wa wagombea.

Hayo yamejiri baada ya wananchi kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi huku ikibainika kwamba mshukiwa aliyekamatwa amewekwa chini ya ulinzi katika kituo cha Polisi cha Webuye
 
Kenya

IEBC yasema haitamtangaza mshindi Urais Kenya​

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati amesema hawatamtaja mshindi wa uchaguzi wa Urais Kenya hii leo licha ya matokeo kuanza kujumlishwa na mawakala vikiwemo vyombo vya Habari vinavyotumia Fomu za 34A zilizopo.

“Matokeo katika tovuti ya umma ni yale yale ambayo tume itatumia kutangaza matokeo pekee, tumewapa mawakala, vyombo vya habari na baadhi ya wadau kupata usawa ila tamko la matokeo ya Urais halitafanyika leo,” amesema Chebukati.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati.
Katika kikao cheke na Hanahabari hivi karibuni kabla ya kupiga kura hapo jana, Mwenyekiti huyo wa IEBC pia alikaririwa akisema matokeo yatakayotangazwa katika vituo vya kupigia kura yatakuwa ya mwisho.

Aidha, Chebukati alibainisha kuwa IEBC bado haijapokea nakala halisi za Fomu 34A au 34B na kuongeza kwamba, “ukusanyaji wa matokeo kutoka maeneo bunge 290 unaendelea na wasimamizi wa uchaguzi watatoa fomu 34B baadaye.”

Hata hivyo, mwenyekiti huyo amezidi kusisitiza kuwa, “Tunawahimiza wagombea ambao wameshindwa katika uchaguzi wakubali matokeo.”

Huku tume ikiwa bado kujumlisha takwimu za urais, matokeo ya muda ya Taifa kulingana na fomu 34A zilizopakiwa kwenye tovuti ya IEBC yanaonyesha kuwa Naibu Rais William Ruto anaongoza kwa asilimia 51.45 na Raila Odinga kwa asilimia 47.9
 
Mbunge wa Kenya ametoweka baada ya kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake Magharibi mwa Kenya.
Walioshuhudia wanadai Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alimpiga mwanamume huyo kichwani wakati wa mabishano katika kituo cha kupigia kura kaunti ya Bungoma.
Polisi sasa wameanzisha msako wa kumtafuta mbunge anayewania muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Wamempa saa 24 kujisalimisha kwa mamlaka zinazochunguza mauaji hayo. Bw Barasa si mgeni katika mabishano.
Mwaka jana, alikamatwa na kushtakiwa kwa kumshambulia mwanamuziki wa nchini humo. Habari zaidi zinasema aliwahi kuhudumu katika jeshi.
Hizi tabia Kumbe zipo nchi nyingi maana huku kwetu Kuna mmoja alimtandika bakora mwenzie hadi akazimia

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom