Katika makundi manne ya watu duniani, inatajwa kwamba, wanadamu wanaopatikana kundi la melancholi, hawa ni kundi linalotajwa kuwa wakipenda wamependa, hawana nafasi ya kuwa na wapenzi makumi kwa mamia, mmoja tu anatosha, na ikitokea akatoswa ni masikitiko ya kutosha na hata anaweza amua kukaa single kwa miaka mingi tu.
Lakini kuna kundi linaitwa sanguine, hao wanatajwa kama wapenda ngono sana, na hawakai na mpenxzi mmoja kwa muda mrefu. Hao ni chapa ilale, na hata akielezwa kuhusu kutoswa ataishia kuitikia tu poa, na waweza mkuta ametoswa asubuhi jioni tayari ana mtu mwingine. Na hao, sanguine ndio unakuta mtaani wanafahamika kama jamvi la wageni(kwa wanawake), na mara nyingi kwa wanawake wa kundi la sanguine, wanatumika kama maji ya kunawia na yale ya kunywa yanapatikana eneo jingine.